Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua kazi ya umaliziaji wa ujenzi wa Uwanja cha Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam, Februari 28,
2019. Ujenzi wa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 95 na unatajiwa
kukabidhiwa kwa serikali Mei mwaka huu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja
cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kusema ameridhishwa
hatua iliyofikiwa.
Mradi wa ujenzi wa jengo hilo
umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, mwaka huu ambapo
hadi sasa tayari maeneo mengi yamekamilika ikiwa ni pamoja na sehemu za
abiria wanaowasili na kuondoka.
Waziri Mkuu ambaye ametembelea
mradi huo (Alhamisi, Februari 28, 2019) amesema amefurahi kukuta michoro
ya wanyama kama tembo, twiga, bahari, minazi na majahazi ambayo ni
alama za nchi.
Kufuatia kukamilika kwa uwanja
huo kwa asilimia 95, Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA) ianze kukamilisha taratibu za kuutumia uwanja huo ili
mkandarasi anapoukabidhi uanze kutumika.
Kadhalika, Waziri Mkuu
ameipongeza kampuni inayojenga uwanja huo kwa kazi nzuri waliyoifanya
kwa sababu jengo ni zuri na linavutia. Pia amewapongeza Watanzania
wanaofanya kazi kwenye mradi huo.
Awali, akisoma taarifa ya mradi
huo, Mkurugenzi wa Walaka wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi
Patrick Mfugale alimuelezwa Waziri Mkuu kuwa jengo hilo limekamilika kwa
asilimia 95.
Mhandisi huyo alisema tayari
wamefanya majaribio ya kwanza ya mifumo na vifaa mbalimbali na kwamba
mkandarasi anatarajia kukabidhi mradi huo Mei 31 mwaka huu. Jengo hilo
linauwezo kubeba abiria milioni sita.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua kazi ya umaliziaji wa ujenzi wa Uwanja cha Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam, Februari 28,
2019. Ujenzi wa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 95 na unatajiwa
kukabidhiwa kwa serikali Mei mwaka huu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Jengo la Uwanja wa Ndege cha
Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28,
2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa
limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei
mwaka huu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

akiaga wakati alipoondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
Terminal Three, jijini Dar es salaam baada ya kukagua ujenzi wa uwanja
huo ambao umekamilika kwa asilimin 95 na unarajiwa kukamilika Mei mwaka
huu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments :
Post a Comment