Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe.Jenista Mhagama akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi hiyo
anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki wakati alipokutana na
watumishi wa Ofisi yake Januari 30, 2019 Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi hiyo
anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akisalimiana na Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde
wakati wa mkutano huo na watumishi wa ofisi yake Januari 30, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi hiyo
anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akisalimiana na Katibu
Mkuu wa Ofisi hiyo Bi. Dorothy Mwaluko.
Waziri wa Nchi Ofisi hiyo
anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akisalimiana na baadhi
ya watumishi wa Ofisi hiyo alipokutana nao Januari 30, 2019 katika Ofisi
hiyo Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na watumishi wa ofisi yake walipokutana
nao mapema hii leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akizungumza na
watendaji wa Ofisi yake (hawapo pichani) walipokutana kuzungumza nao
Jijini Dodoma, kulia ni Waziri wa Nchi ofisi hiyo, (Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama na wa kwanza kushoto
ni Naibu wake Mhe. Anthony Mavunde.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Mhe.Jenista Mhagama
pamoja na Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde wakiwa katika ofisi hiyo
walipokutana na Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu hii leo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akizungumza jambo wakati wa
mkutano wao na Mawaziri wa Nchi wa Ofisi hiyo walipokutana Januari 30,
2019 Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akizungumza jambo na Viongozi wa
Ofisi hiyo alipokutana nao ofisini kwake hii leo, wa kwanza kushoto ni
Waziri wa Nchi ofisi hiyo anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja na Naibu wake
Mhe.Anthony Mavunde.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu wakisubiri kuzungumza na Waziri wa Nchi Ofisi hiyo
anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki alipokutana nao kujadili
masula ya ofisi yao Januari 30, 2019.
………………………………………………………………………………
MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki amekutana na
watumishi wa ofisi yake kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Magufuli kushika wadhifa
huo mpya.
Waziri Kairuki amekutana na
watumishi hao mapema hii leo (Januari 30, 2019) katika Ofisi hiyo Jijini
Dodoma na kuzungumza nao ikiwa ni sehemu ya kufahamiana na kujua ofisi
hiyo.
Mkutano huo uliohudhuriwa na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama pamoja na Naibu wake
Mhe.Anthony Mavunde pamoja na Makatibu wakuu wa Ofisi hiyo Bi.Maimuna
Tarishi anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu pamoja na Dorothy Mwaluko
anayeshughulikia Sera, Uratibu na Uwekezaji.
Kairuki waliwataka watumishi hao
kuendelea kufanya kazi kwa umoja na uzalendo ili kujilete maendeleo
nchini na kuahidi kushirikiano nao kwa kipindi chote atakachokuwa katika
Ofisi hiyo.
“Kipekee ninawashukuru viongozi
na watumishi wote wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mapokezi mazuri na hii ni
ishara ya umoja wenu na ninaahidi kushirikiana na watendaji wote katika
utekelezaji wa majukumu tuliyonayo kwa maslahii mapana ya ofisi yetu
na Taifa kwa ujumla,”alisisitiza Kairuki
Naye Waziri wa Nchi wa ofisi hiyo
Mhe.Jenista Mhagama alipongeza watumishi wa Ofisi yake kwa kuendelea
kutekeleza majukumu na kuwataka kuwa na uzalendo na weledi wa hali ya
juu.
“Ninachoweza kusema tutaendelea
kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa kazi za kila siku kwa kuzingatia
kuwa hii ni familia moja yenye nia moja ikiwa ni kuunga mkono jitihada
za Mhe.Rais ili kujiletea maendeleo katika nchi yetu,”alisema Mhagama.
No comments :
Post a Comment