Meneja wa Jengo la Taasisi ya Moyo
Jakaya (JKCI) Kikwete Bi. Flora Kassembe akimwelezea Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu namna
ambavyo wodi ya watoto itakavyotumika wakati wa ziara fupi ya waziri
huyo kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya
moyo jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuregenzi Mtendaji wa
Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na mtoto
Shakira Athumani kutoka Tanga anayesubiria kufanyiwa upasuaji wa
magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) baada ya
ziara fupi ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto
wenye magonjwa ya moyo jana katika taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Wodi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya
moyo Afrika Mashariki na kati.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza baada ya
kufanya ziara fupi ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya
watoto wenye magonjwa ya moyo jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuregenzi Mtendaji wa Taasisi
hiyo Prof. Mohamed Janabi na kushoto ni Meneja wa Jengo la taasisi hiyo
Bi. Flora Kassembe. Wodi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto
wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja
na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wadau wa
taasisi ya Baps Charity baada ya kufanya ziara katika taasisi hiyo na
kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto jana katika
taasisi hiyo Jinini Dar es Salaam. Wodi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya
kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na baadhi
ya wagonjwa wanaosubiri kupatiwa huduma za matibabu ya moyo baada ya
kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto
wenye magonjwa ya moyo jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
jijini Dar es Salaam. Wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo
inayojengwa katika Taasisi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa
watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto
Loveness Richard anayesubiri kuingizwa katika chumba cha upasuaji wa
moyo kupitia tundu dogo kwa kutumia mtambo wa Cathlab baada ya kufanya
ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye
magonjwa ya moyo jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar
es Salaam. Wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo inayojengwa
katika taasisi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye
magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsikiliza bibi
aliyemfikisha mjukuu wake katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
kwa ajili ya kupata matibabu ya moyo Donata John (kushoto) baada ya
kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto
wenye magonjwa ya moyo jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
jijini Dar es Salaam. Wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo
inayojengwa katika taasisi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa
watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsikiliza mtoto
aliyefanyiwa upasuaji wa moyo kupitia tundu dogo kwenye paja
alipotembelea wodi za wagonjwa wa moyo baada ya kufanya ziara fupi
kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya
moyo jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.
………………………….
Na: Genofeva Matemu – JKCI
Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete
(JKCI) imekuwa taasisi ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kuwa na wodi
pekee ya kuwahudumia watoto wenye magonjwa ya moyo bila kuwachanganya
na watu wazima.
Eneo la wodi hiyo lilitolewa mwaka
2017 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe
Magufuli alipokua akizindua Hospitali ya Mloganzila na kuiagiza
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoa sehemu ya jengo linalohudumia
watoto kwa JKCI ili watoto wenye magonjwa ya moyo waweze kuwa na wodi
yao katika kuleta ufanisi wa matibabu ya moyo kwa watoto hapa nchini.
Akizungumza mara baada ya kufanya
ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi hiyo Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamaii, Jinsi, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alisema
upatikanaji wa wodi hiyo ni juhudi za serikali katika kuhakikisha
utolewaji wa matibabu ya moyo kwa watoto ya kibingwa yanaendelea
kuboreshwa hapa nchini.
“Kwa wodi za watoto wenye magonjwa
ya moyo peke yake kwa hapa Afrika Mashariki na kati hii ndio itakua
wodi ya kwanza inayowahudumia watoto bila kuwachanganya na watu wazima
na hii italeta ufanisi zaidi kwani nafasi ya kufanya makosa haitakuwepo
kwasababu kutakuwa na wataalamu wanaohudumia watoto tu” alisema Waziri
Ummy
Waziri Ummy, alisema wodi hiyo
ambayo ukarabati wake umekamilika inatarajiwa kuwa na vitanda 32 na
chumba cha uangalizi maalum (ICU) kitakachokuwa na vitanda 15 jambo
ambalo litasaidia kuwafanyia upasuaji watoto wengi zaidi waliopo katika
foleni ya upasuaji na kuokoa maisha yao.
“Serikali ilitoa milioni 700 kwa
ajili ya ukarabati wa wodi hii na sasa kwa mara nyingine tena serikali
imetoa milioni 500 kukamilisha miundombinu ya ukarabati wa wodi hii.
Nawashukuru sana taasisi ya Baps Charity ambao nao wamewekeza milioni
800 katika kuhakikisha kuwa wodi hii inakarabatiwa, serikali tutazidi
kuunga mkono juhudi hizi ” alisema Waziri Ummy.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prf. Mohamed, Janabi
alisema kwa shifti mbili za kliniki ya watoto zilizopo JKCI inaona
wagonjwa wa moyo hadi sitini kwa siku thelathini wakiwa ni watoto, hivyo
kulikuwa na umuhimu wa kuongeza wodi hiyo ya watoto.
Akizungumzia upasuaji wa magonjwa
ya moyo prof. Janabi amesema kuwa jumla ya wangonjwa 1356 wamefanyiwa
upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa mwaka 2018, hii
kwa mwaka jana ukiondoa Afrika kusini JKCI ndio hospitali iliyofanya
upasuaji kwa wangonjwa wa moyo wengi zaidi kuliko nchi yoyote ya Afrika.
“Wodi hii mpya ni kwaajili ya
watoto chini ya miaka 13 pekee na hii itatufanya kuwa taasisi ya kwanza
Afrika Mashariki na kati kuwa na jengo lenye kuhudumia watoto bila
kuwanchanganya na watu wazima “alisema prof. Janabi
No comments :
Post a Comment