NJOMBE
Mabomu ya machozi yamelindima
katika viunga vya mji wa Njombe kwa lengo la kuwatanya mamia ya wananchi
waliokuwa wakiandamana kuelekea kituo kikuu cha polisi cha mkoa wa
Njombe wakipinga kitendo cha jeshi hilo kumchukua kinguvu mtu mmoja
waliehisia kuwa mtekaji wa watoto , baada ya kumkuta na mtoto mdogo
akiwa analia katika mtaa wa mgendela ambapo baada ya wananchi kumuhoji
alimuacha mtoto huyo na kutimua mbio.
Wakizungumza na clouds Tv baadhi
ya waandamanaji majira ya saa saba mchana akiwemo Pita Remmy na Anitha
Mgaya wamesema wamechukizwa na kitendo cha jeshi hilo kuendelea kuwafuga
watu hao ambao wamesababisha maisha ya watoto wengi kupotea na kwamba
wanamtaka mtuhumiwa huyo waweze wamshughulikie liwe funzo kwa wengine.
Baada ya kurejea kwa hali ya
amani katika viunga vya mji wa Njombe,naibu waziri wa mambo ya ndani
Mhandisi Hamad Masauni anamtaka kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa
Rashid Ngonyani kueleza sababu ya kupigwa mabomu ambae anasema lengo
lilikuwa kumnusuru mtuhumiwa wa wizi wa bodaboda kauli ambayo inapishana
na inayotolewa na mkuu wa polisi wilaya ya Njombe Kashilaeli Munuo
ambaye amedai mtuhumiwa huyo anahusishwa na utekaji wa watoto.
Mkanganyiko huo unaibua shaka kwa wananchi na kuamua kuweka bayana. Kama ambavyo Alphonce mbulo wanaeleza.
Kufuatia mkanganyiko huo waziri
Masauni anawataka wananchi wanaojua chanzo cha kuibuka kwa taaruki hiyo
na pindi ukweli utakapo bainika aliyetoa taarifa za uongo mbele ya umma
atachukuliwa hatua za kisheria.
Katika maandamano hayo mtu
mwanamke mmoja amejeruhiwa na bomu la machozi katika miguu na kukimbizwa
katika kituo cha afya cha mjini huku hadi sasa watoto tisa na wengine
waliotekwa hawajulikani walipo.
No comments :
Post a Comment