Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista
Mhagama, akisisitiza jambo wakati alipokutana na wajumbe wa Baraza la
Biashara Mkoa wa Kigoma, wakati alipofika mkoani humo kufuatilia
utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa, kulia kwake ni
Mkuu wa mkoa huo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga, Katibu
Tawala wa mkoa huo, Rashid Mchata na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson
Anga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista
Mhagama, akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa Kigoma, Rashid Mchata,
akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Baraza la Biashara la mkoa huo,
wakati Waziri alipofika mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli
za Baraza la Biashara la Taifa,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista
Mhagama, akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Kuboresha Mazingira ya
Biashara na Uwekezaji (LIC), Andrew Mhina akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa Mradi huo mkoani Kigoma, wakati Waziri alipofika mkoani
humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista
Mhagama, akiongea na Mjasiriamali aliyekuwa akihudumiwa katika kituo
cha Biashara (One Stop Business Center) wilayani Kigoma, wakati
alipofika mkoani Kigoma kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la
Biashara la Taifa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista
Mhagama, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la
Biashara la Mkoa wa Kigoma, wakati Waziri alipofika mkoani humo
kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa
……………………………………………………………………………….
Na. OWM, Kigoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama (Mb), ameitaja mikoa 11 ambayo ilianzisha mabaraza ya Biashara
na hadi sasa yako hai na kubainisha kuwa mikoa mingine ilitekeleza agizo
la kuanzisha mabaraza hayo tu lakini utendaji wa Mabaraza hayo umekuwa
siyo endelevu.
Waziri Mhagama ameitaja Mikoa
hiyo 11 ambayo Mabaraza yake yako hai hadi sasa kuwa ni
Dodoma, Kigoma,
Tanga, Geita, Morogoro, shinyanga, Dar es Salaam, Pwani, Iringa, Songwe
na Mbeya. Aidha, Mhagama amebainisha kuwa Mikoa mingine ambayo mabaraza
yake hayafanyi vikao inakiuka Waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2001
unaosisitiza kuanzishwa kwa mabaraza hayo na utendaji wake kuwa
endelevu.
Akiongea wakati wa kufuatilia
utekelezaji wa shughuli za Baraza la Taifa la Biashara mkoani Kigoma,
Waziri Mhagama alifafanua kuwa Dhumuni kuu la kuanzisha mabaraza ya
biashara hususani katika ngazi ya wilaya na mikoa ni kuweka mfumo rasmi
wa kuwakutanisha viongozi wakuu wa Serikali na Sekta Binafsi katika kila
ngazi ya utawala, kujadiliana jinsi ya kuboresha mazingira ya biashara
na uwekezaji nchini kwa ajili ya kukuza sekta binafsi ambayo ndio
muhimili muhimu wa kukuza uchumi wa nchi.
“Hatuwezi kuwa tunamshuhudia Mhe.
Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli anaitisha vikao vya
Baraza la Taifa la Biashara katika ngazi ya Taifa lakini katika ngazi
ya mkoa na wilaya hamtekelezi maagizo hayo, lazima mabaraza yakutane ili
kutatua kero za wafanyabiashara na wawekezaji katika ngazi ya mkoa na
wilaya, lakini pia itasaidia kuibua fursa za uwekezaji na kuzinadi fursa
hizo, na sisi tumeamua kukagua mkoa mmoja baada ya mwingine ili
kupunguza kero za wafanya biashara na wawekezaji” Amesema Mhagama
Wakiongea kwa nyakati tofauti
wakati Waziri Mhagama alipokutana na Wajumbe wa Baraza la Mkoa la
Biashara, Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel
Maganga , Mkuu wa wilaya ya Kigoma, Samson Anga na Katibu Tawala wa Mkoa
huo, Rashid Mchata, walieleza kuwa kupitia Mradi wa Kuboresha
Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (LIC), wameweza kuimarisha mfumo wa
majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi kupitia Mabaraza ya
Biashara ya Mikoa na Wilaya.
Naye Mratibu wa Mradi huo, Andrew
Mhina alibainisha kuwa Mradi huo unalenga kuhakikisha kuwa unaboresha
mazingira ya Biashara na uwekezaji nchini tayari kwa kushirikiana
Baraza la Taifa la Biashara wameandaa mwongozo wa Majadiliano Kati ya
Serikali na Sekta Binafsi ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kuyajengea uwezo
Mabaraza ya Mikoa yaweze kuwa endelevu na yenye ufanisi.
Baraza la Taifa la Biashara
lilianzishwa kwa Waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2001 na kuchapishwa
kwenye Gazeti la Serikali Na. 39 la tarehe 28 Septemba 2001. Baraza
hilo ni jukwaa la majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi,
na lengo kuu la Baraza ni kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji
kwa njia ya majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.Aidha
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara ni Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
No comments :
Post a Comment