Na John Walter-Manyara
Taasisi ya kuzuaia na Kupambana
na Rushwa [TAKUKURU] mkoa wa Manyara kwa kipindi cha Julai hadi Novemba
2018, imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi milioni 270,973,774.48
zilizokuwa zimefanyiwa ujanja ujanja kutoka kwenye miradi mbambali
inayotekelezwa mkoani hapa na kuzirejesha serikalini na zingine
kuzielekeza kwenye miradi husika.
Pia Taasisi hiyo imeanzisha
utaratibu wa kufuatilia fedha zote zinazotolewa na serikali pamoja
na
wafadhili kwa ajili ya huduma na miradi ya Maendeleo kuanzia bajeti
zinapopitishwa,zinapo pokelewa au kukusanywa kutoka vyanzo vya ndani na
kufuatilia mchakato wa matumizi au manunuzi unapofanyika na katika
hatua zote za utekelezaji wa mradi husika.
Akitoa taarifa ya utendaji kazi
wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Mkuu wa TAKUKURU Fidelis Kalungura, amesema
katika ufuatiliaji huo watahakikisha wanadhibiti ucheweleweshaji katika
uanzishaji wa mchakato wa matumizi mara baada ya fedha kupokelewa au
kukusanywa kwani mchakato wa matumizi na manunuzi mara nyingi yamekuwa
yakiathiriwa na vitendo vya rushwa.
Aidha Kalungura amesema TAKUKURU
mkoani Manyara itakuwa makini katika kusimamia hatua ya utekelezaji wa
mradi ili pasitokee uvujaji au uchepuzi na fedha ili kuhakikisha mradi
husika unakamilika ukiwa unalingana na thamani halisi ya fedha
zilizotolewa.
Amesema jumla ya miradi 71 yenye
thamani ya shilingi Bilioni 47.8 inayotekelezwa mkoani Manyara
inafuatiliwa ambapo inajumuisha miradi 48 ya maji,miradi 8 ya
Afya,miradi 9 ya ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu,mradi mmoja [1]
wa ofisi ya Halmashauri ya Kiteto,ujenzi wa jingo moja [1] la mazoezi
VETA,ujenzi wa Ghala la kuhifadhia mazao katika kijiji cha Matufa,mradi
wa mtaa wa viwanda SIDO,mradi wa mtandao wa bara bara awamu ya pili
zenye urefu wa Km. 4.108 pamoja na mradi wa ujenzi wa daraja la Magara.
Mkuu huyo amesema TAKUKURU mkoani
Manyara imejipanga kuzuia Rushwa kwa kufatilia fedha zote zinazotolewa
na serikali,wafaadhili na zitokanazo na makusanyo ya ndani kwa ajili ya
huduma na maendeleo, na kuongeza kuwa itaendelea kushirikiana na jamii
katika mapambano ya rushwa pamoja na kutatua kero mbalimbali za wananchi
zinazohusiana na Rushwa.
No comments :
Post a Comment