RAIS wa 41 wa Marekani, George Herbert Walker Bush, amefariki dunia jana, Ijumaa, Novemba 30, 2018, majira
ya saa 4:10 usiku mjini Houston akiwa na umri wa miaka 94, msemaji wake
Jim McGrath amethibitisha kifo chake na kusema chanzo chake kimetokana
na tatizo la mapafu (pneumonia) lililokuwa likimsumbua kwa muda mrefu.
Shujaa huyo wa Vita vya Pili vya
Dunia ambaye alizaliwa Juni 12, 1924, ni rais aliyeongoza kwa
awamu
moja tu akiingia madarakani mwaka 1989 na kuondoka 1993 hivyo kubaki
kama rais pekee aliyeiongoza Marekani kwa awamu moja.
Bush ambaye pia ni babaye rais wa 43
wa Marekani, George W Bush, amewahi kuwa rubani katika Jeshi la
Marekani, Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na Makamu wa
Rais.
Mzee Bush amefariki ikiwa ni miezi saba tu tangu kifo cha aliyekuwa mkewe, Barbara Bush ambaye alifariki dunia Aprili 17, 2018, huko Huston akiwa na umri wa miaka 73.
Kwa upande wa siasa za nje, matukio
makubwa yaliyofanyika duniani wakati wa utawala wake ni pamoja na
kuanzishwa kwa Vita vya Ghuba, kuanguka kwa Ukuta wa Berlin (nchini
Ujerumani) na kuvunjika kwa Muungano wa Kisoviet.
Mambo mengine yaliyofanyika nchini
Marekani chini yake ni pamoja na kupigwa marufuku kwa uingizaji wa
bunduki za ‘semi-automatic’ nchini humo na kusainiwakwa Sheria ya 1990
ya Wamarekani wenye Ulemevu na ya 1991 ya Haki za Kiraia.
Hata hivyo, pamoja na kusema wakati wa kampeni za kuchaguliwa kwake kwamba hapangekuwa na kodi mpya wakati wa utawala wake, jambo hilo hakulifanya.
Baba yake George, aliyeitwa Prescott, alikuwa seneta, na mwanaye mkubwa wa kiume, akawa rais wa 43 wa Marekani.
Ameacha watoto watano, wajukuu 17 na vitukuu wanane. Pia alikuwa na
binti aliyeitwa Robin ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka mitatu
kutokana na kansa ya damu.
No comments :
Post a Comment