Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi katika ziara
ya siku mbili ya kutatua kero za wananchi mara baada ya kusikiliza
malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Bugombe kilichopo wilaya
ya Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya
katika kijiji cha Bugombe wakiomba waruhusiwe kutengeneza barabara
ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Maisome ili kupunguza adha ya usafiri kwa
wananchi hao.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe.
Dkt. Charles Tizeba akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara
katika ziara ya siku mbili ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.
Constantine Kanyasu aliyoifanya ya kutatua kero za wananchi wa kijiji
Bugombe wilaya ya Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara
uliofanya katika kijiji cha Kisaba na Bugombe
Baadhi ya wananchi waliohudhuria
mkutano wa hadhara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Constantine Kanyasu wakati alipofanya ziara ya kutatua kero za
wananchi wa kijiji cha Kisaba na Busikimbi vilivyopo wilaya ya
Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya katika
kijiji cha Bugombe.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Bugombe
akizungumza na na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika ziara ya
siku mbili ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine
Kanyasu aliyoifanya ya kutatua kero za wananchi wananchi wa kijiji
cha Bugombe vilivyopo wilaya ya Sengerama mkoani Mwanza wakati wa
mkutano wa hadhara uliofanya katika kijiji cha Kisaba na Bugombe
Daniel Serengeti ni mkazi wa
kijiji cha Kisaba ambaye shamba lake limemegwa amemuomba Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amsaidie ili shamba lake
lweze kurudishiwa kwa vile yeye ni mmiliki halali
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa amepanda kwenye bodaboda ukiwa
ndo usafiri pekee unaotumika katika kijiji cha Bugombe ambayo ni kambai
ya uvuvi kutokana na kukosekana kwa barabara ya kuweza kupita magari.
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA)
………………………
NA LUSUNGU HELELA-MWANZA
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Constantine Kanyasu ameiagiza Halmashauri ya wilaya Buchosa
mkoani Mwanza kupitia upya ramani ya vijiji vilivyopo ndani ya Hifadhi
ya Msitu wa Kisiwa cha Maisome kwa ajili ya kutatua mgogoro wa
ardhi uliopo kati ya wanavijiji na Halmashauri hiyo.
Ameuagiza Uongozi wa
Halmashauri hiyo ushirikiane na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS) wakati wa inapofanya upya mapitio ya ramani hiyo ili kuweza
kumaliza tatizo la mgogoro huo uliopo kufuatia baadhi ya maeneo ya
wananchi kuingia ndani ya Hifadhi ya
msitu huo kwa mujibu ramani
iliyopo.
Ametoa agizo alipokuwa
wilayani humo kwa ziara ya siku mbili ya kutatua kero za wananchi mara
baada ya kusikiliza malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Kisaba
na Busikimbi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya katika kijiji cha
Kisaba wakidai kuwa TFS imechukua baadhi ya maeneo ya vijiji hivyo.
Katika vijiji hivyo jumla ya
ekari 103 za wananchi walizokuwa wakizitumi katika shughuli za
kiuchumi zinadaiwa kuingia ndani ya Hifadhi ya msitu iliyo chini ya TFS
Naibu Waziri Kanyasu
amefafanua kuwa hakuna mgogoro kati ya TFS na wananchi ila kuna mgogoro
kati ya wananchi na Halmashauri waliotengeneza ramani hiyo na sio TFS.
Daniel Serengeti ni mkazi wa
kijiji cha kisaba ambaye shamba lake limemegwa ameiomba serikali
kuwarudishia maeneo hayo kwa kuwa walikuwa wanayamiliki tangu mwaka
1968.
‘’ wachora ramani sio TFS,
Hivyo TFS wanatumia ramani iliyokwisha tengenezwa na Halmashauri hiyo
kutokana na hilo wanatakiwa kupitia upya na kuondoa mgogoro,alisema
.Kanyasu.
Mkurugenzi wa halmashauri ya
Buchosa Crispin Luanda amesema kuwa maagizo hayo atayatekeleza kwa
wakati ili kufanikisha swala hilo .
Amesema mara baada ya ramani
mpya itakapokamilika itapelekwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili
ya urekebishaji wa maeneo hayo.
Katika hatua nyingine,
Kanyasu ameruhusu upanuzi wa njia itakayopita ndani ya Hifadhi ya
Maisome kwa ajili ya kuwapunguzia adha wakazi walio wengi wanaokwenda
katika Kambi ya Uvuvi ya Bugombe kwa ajili ya kujipatia mahitaji muhimu
ya kila siku.
Mbunge wa jimbo la Buchosa Dk
Charles Tizeba amemshuru naibu wa Waziri huyo kwa kutatua mgogoro huo
ambao ulikuwa kero kwa wananchi.
No comments :
Post a Comment