Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo
(katikati) akiwasili na kupokelewa na Mkuu wa kitengo cha Elimu katika
shirika la UNESCO, Bi. Faith Shayo (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Elimu
ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu Sayansi na
Teknolojia, Dk. Noel Mbonde wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear
ll na warsha ya kiufundi iliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard
jijini Dar es Salaam.
Ofisa
Balozi mdogo wa Ubalozi wa Korea nchini, Bi. Jiin An (kulia)
akibadilishana mawazo na Mkuu wa kitengo cha Elimu katika shirika la
UNESCO, Bi. Faith Shayo (kushoto) wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa
Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea
Courtyard jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mratibu wa mradi wa BEAR ll,
kutoka makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na
Utamaduni (UNESCO) Bw. Whan Sik Kim.
Mratibu
wa mradi wa Bear II nchini, Bi Andulile Daudi (kushoto) akibadilishana
mawazo na Ofisa aneyshughulikia uratibu wa ushirikiano ufundi stadi
kati ya Tz na Ujerumani kutoka Handwerkskammer jijini Hamburg, Bw Frank
Glucklich (katikati) pamoja na Mshauri kutoka Handwerkskammer jijini
Hamburg, R. Nicolas Udewald wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear
ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard
jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa kitengo cha Elimu katika shirika la UNESCO, Bi. Faith Shayo akitoa
neno la ukaribisho kwa meza kuu na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa
Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea
Courtyard jijini Dar es Salaam.
Kutoka
kushoto ni Mratibu wa mradi wa BEAR ll, kutoka makao makuu ya Shirika
la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Whan Sik
Kim, Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco, Dr. Hamisi Malebo,
Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya
Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Noel Mbonde, Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo, Ofisa Balozi mdogo wa
Ubalozi wa Korea nchini, Bi. Jiin An pamoja na Mratibu wa mradi wa BEAR
II kutoka ofisi za Unesco Nairobi, Bw.Teeluck Bhuwanee
Mkurugenzi
wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu
Sayansi na Teknolojia, Dk. Noel Mbonde akizungumzia mradi wa BEAR II
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll
na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard
jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo
akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll na warsha ya
kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es
Salaam.
Ofisa
Balozi mdogo wa Ubalozi wa Korea nchini, Bi. Jiin An akitoa salamu za
serikali ya Korea Kusini kwa niaba ya Balozi wa Korea Kusini, Mh. Geum
Young Song wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll na warsha ya
kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es
Salaam.
Mratibu
wa mradi wa BEAR II kutoka ofisi za Unesco Nairobi, Bw.Teeluck Bhuwanee
akitoa neno kwa niaba ya Unesco wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa
Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea
Courtyard jijini Dar es Salaam.
Injinia
Enock Kayani kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia akiwasilisha
mpango kazi wa mwaka mmoja ulioandaliwa na kamati ya kifundi wakati wa
kufunga mafunzo ya siku tatu ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi
yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wadau kutoka MoEST, Wizara wa Kilimo, UNESCO, NACTE, TCCA, ATE, VETA
pamoja wadau wa maendeleo walioshiriki halfa ya kufunga mafunzo ya siku
tatu ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika
hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard
Akwilapo pamoja na washiriki wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa BEAR
ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea
Courtyard jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja. BEAR ll ni
mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
Na Mwandishi Wetu
KATIBU
Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo
ameshukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni
(UNESCO) na Ubalozi wa Korea Kusini kwa kufanikisha warsha inayoandaa
mpango kazi kwa walimu na wadau wanaosimamia mafunzo ya ufundi stadi.
Akizungumza
wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll Katibu Mkuu huyo alisema
wakati taifa linaelekea katika uchumi wa viwanda mradi huo na mafunzo
yake ni kitu muhimu sana.
Mafunzo
hayo ya siku tatu yalijadili namna ya kufikisha elimu ya ufundi stadi
inayooana na mahitaji halisi ya nguvu kazi katika jamii.
Mafunzo
hayo yalilenga kutambua na kusaidia kufanikisha malengo matatu ya
matumizi ya ufundi stadi yanayozingatia mahitaji ya uchumi, kuboresha
mafunzo ya ufundi stadi kwa wateja na kuboresha hali ya uelewa wa
ufundi stadi miongoni mwa vijana na wananchi.
Katibu
mkuu huyo alisema kwamba serikali inajivunia hatua iliyofikiwa ya mradi
huo wa Bear ll ya uandazi wa mpango kazi wa mwaka mmoja na wa miaka
mitatu ambao kwa sasa unasubiri kamati ya wizara kuupitia na kuubariki.
Alisema
kwamba Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itahakikisha kwamba mradi
huo wa Bear ll unatekelezwa na kutoa matunda yanayotarajiwa.
Katika
warsha hiyo mada kadhaa ziliwasilishwa ikiwamo mkakati wa UNESCO kuhusu
ufundi stadi na historia ya mradi wa Bear II ambao unapoletwa nchini
Tanzania upo katika awamu ya pili.
Mradi
huo wa Bear ll unafanyika katika nchi tano zikiwamo Tanzania na Uganda
katika awamu yake ya pili. Nchi zingine ni Ethiopia, Kenya na
Madagascar.
Kwa
mujibu wa taarifa za kitafiti kuna malalamiko kwamba wahitimu wa ufundi
stadi wanashindwa kwenda sanjari na matakwa ya shughuli zao katika
viwanda.
Mradi
huo wa dola za Marekani milioni 1.56 unatarajiwa kugusa mamlaka
mbalimbali za mafunzo nchini yakiwemo mafunzo ya ufundi stadi
zitakazowezesha wafundishaji kutoa mwanga unaotakiwa kwa mafundi stadi.
Mamlaka hizo ni pamoja na TCU, Nacte, Baraza la Ithibati nakadhalika.
Wakati
wa uzinduzi wa mradi huo Balozi wa Korea Kusini Geum- Young alisema
taifa lake litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha
kwamba linawezesha elimu ambayo ni msingi mkubwa wa maendeleo ya
viwanda.
Naye
Mkuu wa kitengo cha cha elimu katika shirika la UNESCO Faith Shayo
alisema kwamba lengo kubwa la mradi huo ni kuboresha mafunzo ya ufundi
nchini na kuweka uwiano wa masomo hayo ili kuhakikisha kwamba
yanachangia katika ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini.
Mratibu
wa BEAR II Bw.Teeluck Bhuwanee alisema ni matumaini yake kwamba
ushirikiano kati ya serikali, Korea Kusini na Unesco utasaidia kuboresha
elimu ya ufundi nchini.
Kuzinduliwa
kwa BEAR II kunaashiria utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kuendeleza
utaalamu (NSDS) kuanzia mwaka 2016/17 hadi 2025/26 wenye lengo la kuwa
na wafanyakazi wataalamu na wenye ushindani.
No comments :
Post a Comment