Balozi
wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima (kushoto) akimsikiliza
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni
msuluhishi wa mgogoro wa Burundi. Rais Mkapa aliwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Entebbe asubuhi ya tarehe 19 Novemba 2018 kwa ajili ya
kuwasilisha ripoti ya mkutano wa upatanishi uliofanyika hivi karibuni
jijini Arusha kwa Mpatanishi Mkuu wa mgogoro huo Rais wa Uganda, Mhe.
Yoweri Kaguta Museveni.
Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni
msuluhishi wa mgogoro wa Burundi akiwa katika chumba cha wageni maalum
katika uwanja wa Ndege wa Entebbe leo. kulia ni Mwambata Jeshi wa
Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda, Brig Gen. Mkumbo, kushoto ni Msaidizi
wa Rais Mkapa katika utatuzi wa mgogoro huo, Balozi David Kapya na
anayemfuatia ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima.
Mhe. Mkapa akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mlima, Balozi Kapya na Bw. Makocha Tembele ambaye ni Katibu wa Rais Mkapa.
No comments :
Post a Comment