Meneja masoko wa Startimes Davis
Malisa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa
wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya kabambe kabisa awa wateja wao
pendwa kwenye msimu huu wa Krismasi uliofanyiaka jijini Dar es Salaam.
Meneja Maudhui wa Startimes
Zamaradi Nzowa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau
mbalimbali wa tasnia ya Filamu pamoja na muziki wa kuhusu maudhui
zitakazopatikana kwenye vifurushi vya Startimes wakati wa uzinduzi wa
promosheni mpya kabambe kabisa awa wateja wao pendwa kwenye msimu huu wa
Krismasi uliofanyiaka jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Benchmark
Production, Rita Paulsen akizungumza kuhusu Startimes wanavyoshirikiana
kwenye kuibua vipaji vya wasanii wachanga wakati wa uzinduzi wa
promosheni mpya kabambe kabisa awa wateja wao pendwa kwenye msimu huu wa
Krismasi uliofanyiaka jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja
……………………
“…Kwa wateja wetu pendwa
kabisa, na wale ambao bado hawajajiunga na familia ya StarTimes inayokua
kila siku, msimu huu wa siku kuu tunawaletea ‘LIPA TUKUBUSTI’ambayo
inakupatia faida nne. Katika kila utakachonunua kutoka kwetu basi sisi
tutakuBUSTI ama tutakuongezea.”
Dar es Salaam Novemba 14, 2018.
Kampuni ya Star Media (T) Ltd
kupitia chapa yake ya StarTimes wametangaza ujio wa Promosheni ya LIPA
TUKUBUSTI katika msimu huu wa Siku Kuu. Promosheni hiyo imezinduliwa
Alhamisi ya wiki hii kwatika Ukumbi wa Terrace, Slipway Masaki jijini
Dar es Salaam na kuhudhuriwa na waigizaji maarufu wa Bongo Movie pamoja
na wasanii wa Muziki wa kizazi Kipya.
Katika Promosheni ya LIPA
TUKUBUSTI wateja wa StarTimes watakuwa wakipatiwa vifurushi vikubwa
zaidi kila watakapolipia na kujiunga na vifurushi vyao vya kawaida kwa
malipo ya mwezi Mzima. Hali kadhalika kwa wateja wapya watapatiwa Antena
BUREE kila watakaponunua king’amuzi cha Antenna kwenye maduka na
mawakala wa StarTimes.
“Vifurushi vyetu, kwa wateja wa
Antenna Ukilipia kifurushi cha NYOTA kwa Tsh 8,000/= utapata kifurushi
cha MAMBO kwa mwezi mzima, Ukilipia kifurushi cha MAMBO kwa Tsh 14,000/=
tutakuBUSTI hadi kifurushi cha UHURU kwa mwezi mzima, na ukilipia UHURU
utapatiwa wiki moja BUREEE!!”. Ndg David Malisa Meneja Masoko wa
StarTimes
“Ving’amuzi vyetu, pata Antena ya
BURE ukinunua king’amuzi cha Antenna kwa Tsh 99,000/= tu, au furahia
kifurushi cha SUPER mwezi mzima BUREEE utakaponunua king’amuzi cha Dish
wa Tsh 106,000/= tu. Huu ndio wakati sahihi zaidi kwa wewe ambaye bado
hujajiunga nasi kununua king’amuzi chako, kwani unapataza ZAIDI kila
unapolipia”. Aliongeza Bw. Malisa.
Sio hivyo tu bali kupitia
promosheni ya LIPA TUKUBUSTI wateja watanufaika kwa Kupata DISH la
BUREEE kila watakaponunua luninga za Kidigitali za StarTimes za ukubwa
wowote ule kuanzia Inchi 24, 32, 43 hadi ile Luninga Smati ya Inchi 55.
Kwa upande wa maudhui, Msimu huu
wa Siku Kuu StarTimes wamejipanga vilivyo kwani wanaleta Filamu Mpya
kabisa za Bongo Movie zilizosheheni mastaa wakali, Huku shindano la
Bongo Star Search likiendelea, na kufikia hatua ya mchujo ndani ya
Studio, Shindano hilo linaendelea kuonekana Kila siku saa tatu Usiku
kupitia chaneli ya StarTimes Swahili Pekee.
“Tuna furaha kubwa kuwaletea
filamu za Bongo Movie Mpya kabisa kwa mwezi mzima wa Disemba, filamu
ambazo zina mastaa tunawaowapenda na kuwafatilia kila siku. Ni wakati wa
kutengeneza kumbukukumbu nzuri na wale tuwapendao na StarTimes
inalifanikisha hilo. Sio hayo tu bali tunaleta Msimu mpya wa Coppa
Italia kwa mara ya kwanza kupitia StarTimes pekee, utamshuhudia
Cristiano Ronaldo na Juventus kuanzia Disemba 5 kupitia chaneli zetu za
Michezo”. Zamaradi Nzowa Meneja Maudhui, StarTimes.
Pia ligi ya Bundesliga
inayoonyeshwa na StarTimes pekee, inaendelea sambamba na ligi ya
Ufaransa maarufu kama Ligue 1, huku zikichagizwa na Ligi ya EUROPA. Bila
kusahau chaneli na vipindi vya watoto kama Jim Jam, POP na chaneli mpya
ya ST Kids vitahakikisha watoto wako wanakuwa na siku kuu ya kipekee.
Kuhusu StarTimes
StarTimes ni kampuni ya Matangazo
ya kidigitali inayoongoza Africa, ikihudumia zaidi ya wateja milioni 10
katika bara zima. StarTimes inamiliki jukwaa la maudhui lenye chaneli
zaidi ya 480 zikiwemo chaneli za Habari, filamu, tamthiliya, michezo,
burudani, vipindi vya watoto, mitindo, dini na vingine vingi. Matazamio
ya Kampuni ni “Kuhakikisha kila familia ya kiafrika inapata, inamudu,
inatazama na kushiriki kwenye Uzuri wa Televisheni ya kidigitali”
No comments :
Post a Comment