Msanii maarufu wa muziki wa
Taarabu Khadija Oumar Kopa akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
DStv ya msimu wa sikukuu ijulikanayo kama “Muda wa Kukiwasha na DStv”
uliofanyika katika ofisi za MultiChoice Tanzania. Katika msimu huu wa
sikukuu ambapo watu wengi hujumuika na familia zao kwa mapumziko ya
mwisho wa mwaka, MultiChoice Tanzania imetangaza ofa kabambe kwa wateja
wake na wale wanaojiunga na huduma za DStv
Meneja Masoko wa MultiChoice
Tanzania Alpha Mria akitambulisha kampeni mpya ya DStv ya msimu wa
sikukuu ijulikanayo kama “Muda wa Kukiwasha na DStv” uliofanyika katika
ofisi za MultiChoice Tanzania. Katika msimu huu wa sikukuu ambapo watu
wengi hujumuika na familia zao kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka,
MultiChoice Tanzania imetangaza ofa kabambe kwa wateja wake na wale
wanaojiunga na huduma za DStv
Meneja Mauzo wa MultiChoice
Tanzania Salum Salum akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya
DStv ya msimu wa sikukuu ijulikanayo kama “Muda wa Kukiwasha na DStv”
uliofanyika katika ofisi za MultiChoice Tanzania. Katika msimu huu wa
sikukuu ambapo watu wengi hujumuika na familia zao kwa mapumziko ya
mwisho wa mwaka, MultiChoice Tanzania imetangaza ofa kabambe kwa wateja
wake na wale wanaojiunga na huduma za DStv
……………………………………………………………………………….
DStv yatangaza neema kwa wateja wake msimu huu wa sikukuu!
Katika msimu huu wa sikukuu
ambapo watu wengi hujumuika na familia zao kwa mapumziko ya mwisho wa
mwaka, MultiChoice Tanzania imetangaza ofa kabambe kwa wateja wake na
wale wanaojiunga na huduma za DStv kupitia kampeni yake maalum
ijulikanayo kama ‘Ni Muda wa Kukiwasha na DStv’.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
kampeni hiyo, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria amesema
wateja wa DStv sasa watapata burudani zaidi za kusisimua kupitia Soka,
Filamu, Tamthilia, Katuni na vipindi mbali mbali vya watoto
vitakavyoileta familia pamoja na kuimarisha upendo.
Kwa mujibu wa Alpha, zaidi ya
maudhui hayo yote yaliyotajwa hapo juu; Katika kunogesha sikukuu,
maudhui mapya yatayoongezwa ndani ya DStv. Maudhui hayo ni pamoja na
tamthilia ya Kapuni ambayo inaingia msimu wake wa pili katika chaneli ya
Maisha Magic Bongo (MMB), Chaneli maalum (EA Movies) yenye mkusanyiko
wa filamu bora za Afrika Mashariki, na pia sinema maalum za watoto
katika chaneli ya Mnet inayojulikana kama Mnet ANIMANIA pamoja
na vipindi mbalimbali vinavyohusiana na msimu huu wa sikukuu. Aidha
Alpha alisisitiza kuwa, Kipindi hiki cha sikukuu kupitia chaneli ya
Maisha Magic Bongo (MMB) itawaletea wateja maudhui mapya na ya kusisimua
zaidi hivyo kuwasihi watanzania wakae tayari kupokea kitu kipya kutoka
MMB tarehe 14 Disemba 2018.
Amesema DStv imekuwa mara kwa
mara ikiwatunuku wateja wake waliopo na wapya zawadi na ofa kabambe huku
wakiendelea kupata burudani ya uhakika muda wote. “Mwaka huu kama
kawaida umekuwa mwaka wa neema kwa wateja kwani tumekuwa na mfululizo wa
zawadi kwa wateja wetu”
Kwa wateja wapya wanaojiunga na
DStv msimu huu watapata ofa maalum ya kuunganishwa kwa shilingi 79,000
pamoja na zawadi maalum ya kifurushi cha mwezi cha Bomba bila malipo ya
ziada. Ofa hii itaendelea kwa muda wa miezi miwili kuanzia tarehe 15
Novemba 2018 na ni kwa nchi nzima.
Akifafanua kuhusu ofa hiyo, Mkuu
wa Mauzo wa kampuni hiyo Salum Salum, amesema kuwa ofa hii ni zawadi ya
kufunga mwaka kwa wateja wapya wa DStv kwani katika kipindi cha miezi
miwili wataweza kuunganishwa na DStv kwa gharama ya shilingi 79,000 tu
na zaidi ya hapo kupewa kifurushi cha Bomba cha mwezi mmoja bila malipo
ya ziada.
“Mbali na kuongezwa kwa chaneli
na maudhui kedekede kwa wateja walipo wa DStv, pia kwa wale ambao bado
hawajajiunga hatujawasahau, sasa tunawapa ofa hiii kabambe ya kujiunga
kwa gharama nafuu na zaidi ya hapo wapate kifurushi cha mwezi mmoja bila
malipo. Hii ni zawadi yetu ya sikukuu kwa wateja wetu” alisema Salum
Salum.
Amesisitiza kuwa ofa hii ni kwa
nchi nzima na tayari wameshajipanga na mawakala wote kuhakikisha kuwa
ofa hii inapatikana nchi nzima. “Mtu yeyote asiwe na wasiwasi wa jinsi
ya kuunganishwa kwa ofa hii. Tunao mawakala wetu wa usambazaji na ufundi
nchi nzima, hivyo hata walio maeneo ya vijijini huduma hii watapata.
No comments :
Post a Comment