Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa maelezo
kwa Kaimu Balozi wa Misri nchini Bibi. Nevine El-Saeed na Mkuu wa Idara
ya Uchumi katika ubalozi huo Bw. Mohamed Ibrahim katika ofisi ndogo za
wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel Kaimu Balozi
wa Misri nchini Bibi. Nevine El-Saeed na Mkuu wa Idara ya Uchumi katika
ubalozi huo Bw. Mohamed Ibrahim, wakati akiongoza kikao cha namna bora
ya uwekezaji wa serikali ya Misri katika sekta ya mifugo nchini (wajumbe
wa mkutano huo hawapo pichani).
Wajumbe wa kikao kuhusu nia ya
serikali ya Misri kuwekeza katika sekta ya mifugo nchini wakifuatilia
mazungumzo ya kikao hicho. Wajumbe hao wanatoka idara zilizo chini ya
Wizara ya Mifyugo na Uvuvi, Dawati la Sekta Binafsi, Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT) na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.
Kaimu Balozi wa Misri nchini
Bibi. Nevine El-Saeed akisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof.
Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) wakati akifafanua namna bora ya
uwekezaji wenye tija kwa nchi zote mbili.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea andiko
la awali la nia ya serikali ya Misri kuwekeza nchini katika sekta ya
mifugo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Uchumi katika ubalozi wa Misri hapa
nchini Bw. Mohamed Ibrahim.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel, Kaimu Balozi
wa Misri nchini Bibi. Nevine El-Saeed na Mkuu wa Idara ya Uchumi katika
ubalozi huo Bw. Mohamed Ibrahim mara baada ya kuahirishwa kwa kikao
kinachohusu nia ya serikali ya Misri kuwekeza katika sekta ya mifugo
nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika
picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Misri nchini Bibi. Nevine El-Saeed,
Mkuu wa Idara ya Uchumi katika ubalozi huo Bw. Mohamed Ibrahim na
wajumbe waliohudhuria
kikao kujadili nia ya serikali ya Misri kuwekeza
katika sekta ya mifugo. Kikao kimefanyika katika ofisi ndogo za wizara
hiyo Jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amefanya
mazungumzo na Kaimu Balozi wa Misri hapa nchini Bibi. Nevine El-Saeed
pamoja na kupokea andiko la awali la nia ya serikali ya Misri kutaka
kuwekeza nchini katika sekta ya mifugo.
Kaimu Balozi wa Misri ambaye
ameambatana na Mkuu wa Idara ya Uchumi katika ubalozi huo Bw. Mohamed
Ibrahim katika ofisi ndogo za wizara ya mifugo na uvuvi zilizopo jijini
Dar es Salaam, amesema serikali ya nchi hiyo inahitaji kuwekeza ili
kufungua fursa mbalimbali ambazo zitapatikana kupitia uwekezaji huo.
Akizungumza na maafisa hao pamoja
na wajumbe waliohudhuria kikao hicho, Katibu Mkuu Ole Gabriel amesema
nchi ya Tanzania ina mifugo mingi na kwamba ikitumika vizuri kupitia
uwekezaji, ambapo nia ya serikali ya awamu ya tano imejikita zaidi
kupitia kufufua na kuanzishwa kwa viwanda vipya kutaongeza fursa nyingi
zaidi zikiwemo za ajira.
Aidha, amesema nia yake ni
kuhakikisha anasimamia nia ya serikali ya Misri kufanikisha uwekezaji
huo ambao anasema wizara yake itahakikisha inaweka mazingira
yatakayofanya uwekezaji huo uwe endelevu na kuleta tija kwa nchi zote
mbili.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na
wakuu wa idara zilizo chini ya ofisi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi,
wawakilishi kutoka Dawati la Sekta Binafsi, Kampuni ya Ranchi za Taifa
(NARCO), Kituo cha Kuendeleza kilimo Nyanda za juu Kusini (SAGCOT) na
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.
No comments :
Post a Comment