Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (Mb) akizungumza na
wadau wa maendeleo ya vijana walipokuta kujadili Sera ya Taifa ya
Maendeleo ya Vijana hii leo Novemba 30, 2018, Kilimani Landmark, Jijini
Dodoma.
Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw.
Andrew Massawe akielezea jambo kwa wadau wa Maendeleo ya Vijana
walioshiriki Mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akiteta jambo na
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akifafanua jambo
kwa wadau wakati wa mkutano huo.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Alex Rutta akielezea jambo wakati wa mkutano huo
Baadhi ya wadau wa maendeleo ya
vijana wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na
Ajira Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa
majadiliano ya rasimu ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana.
Katibu Mkuu UNA Tanzania Bw. Reynald Maeda akichangia hoja wakati wa mkutano huo
Baadhi ya wadau wa maendeleo ya
vijana wakijadiliana kwa pamoja juu ya namna bora ya kuboresha rasimu ya
sera ya maendeleo ya vijana.
Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw.
Andrew Massawe akizungumza jambo na mmoja wa wadau wa maendeleo ya
vijana mara baada ya kufungua mkutano huo. (Kulia) ni Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akiwa kwenye picha ya
pamoja na wadau wa maendeleo ya vijana ikiwemo Wizara za kisekta, Idara
za Serikali, Taasisi za Umoja wa Mataifa, Asasi za kirai, Vyama vya
Siasa vyenye sajili, Taasisi za dini na Vyuo vya elimu ya juu na kati
walipokuta kujadili Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU
…………………….
Na Mwandishi Wetu,Dodoma
Sera ya Maendeleo ya Vijana ya
mwaka 2007 itakayofanyiwa marekebisho hivi karibuni inategemewa kutatua
changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana hasa katika jitihada za
kuwawezesha kujitegemea.
Hayo yamezungumzwa leo jijini
Dodoma na Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana na
Ajira,Anthony Mavunde alipokuwa akifungua majadiliano ya wadau wa vijana
juu ya Rasimu ya Sera Mpya ya Maendeleo ya Vijana.
Mavunde amesema kuwa maendeleo na
ustawi wa vijana nchini ni jambo la muhimu hivyo lazima kuwe na Sera
bora inayotoa muongozo kwa ajili ya utekelezaji wa mipango na mikakati
mbalimbali ya vijana.
“Sera hii itatoa dira yenye
muelekeo wa kuhakikisha Taifa linakua na vijana wenye nguvu, uwezo na
ari ya kushiriki katika nyanja za kimaendeleo zitazokuza uchumi wa nchi
hivyo wajibu mkubwa wa Serikali ni kuweka mazingira wezeshi kwa kuandaa
sera shirikishi, mikakati inayotekelezeka na sheria ambayo ni rafiki kwa
maendeleo ya vijana”, alisema Mavunde.
Mavunde ameongeza kuwa Sera hiyo
itajenga msingi mkubwa katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya mwaka 2020
hadi 2025 ambapo malengo yake makubwa ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya
uchumi wa kati kupitia viwanda ikiwa ni falsafa inayosisitizwa na
Serikali ya Awamu ya Tano.
Amefafanua kuwa hakuna nchi yoyote
Duniani ambayo itaweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo kama haitawekeza
kwenye kundi kubwa la vijana na ndio maana Serikali imeona umuhimu wa
kupitia upya sera hiyo kulingana na matakwa ya Dunia.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa
ofisi hiyo, Andrew Massawe amesema kuwa lengo la kufanya mkutano huo ni
kuwawezesha wadau wa maendeleo ya vijana nchini kutoa maoni ya pamoja na
mkakati wa utekelezaji wa sera hiyo.
“Sera hiyo mpya itawasaidia vijana
kwenda sambamba na mabadiliko mbalimbali yanayotokea yakiwemo ya kisera
na kijamii ili waweze kuendana na ulimwengu wa sayansi na teknolojia”,
alisema Massawe.
Zoezi hilo la ukusanyaji maoni juu
ya urekebishaji wa sera hiyo ulianza tangu mwaka 2015 ambapo wadau
mbalimbali nchini wakiwemo wa Asasi za ndani na za kimataifa,Wizara na
Taasisi mbalimbali, Vyama vya Siasa na Viongozi wa dini.
No comments :
Post a Comment