Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Afrika
Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni pamoja na Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta baada ya viongozi hao kukutana kwenye Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa (AICC) jijini Arusha. Kikao cha 20 cha Wakuu wa nchi za
Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC), ambacho ikuwa kifanyike leo Novemba 30, 2018
kimeahirishwa hadi Desemba 27, 2018 baada ya "koramu" kutotumia kufuatia
Rais wa Burundi, Mhe. Pierre Nkurunzinza kushindwa kuhudhuria,
Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo, Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta
Museveni aliwaambia waandishi wa habari.
Rais
wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa
Uganda
Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museven ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa wa
JUmuoiya ya Afrika Mashariki (EAC), kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa
20 wa
Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC) Novemba 30,2018. Hata hivyo
mkutano huo ulishindwa kufanyika baada ya "koram" kutotimia kufuatia
mwananchama mmoja Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza kushindwa
kuhudhuria. Kwa mujibu wa Rais Museveni mkutano huo sasa utafanyika
Desemba 27, 2018.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Mheshimiwa
Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa
Jijini Arusha(AICC) .Novemba 30,2018.(PICHA NA IKULU)










No comments :
Post a Comment