Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wiki hii ameendelea na
ziara yake ya kutembelea Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Serikali
ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kujitambulisha rasmi na kuboresha
mahusiano baina ya Benki ya CRDB na taasisi hizo.
Katika
mikutano tofauti iliyofanyika siku ya Jumanne, Jumatano na Alhamisi
wiki hii, Nsekela alimtembelea Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini,
Jenerali Venance Mabeyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa nchini, Kamishna Diwani Athumani na Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Siang’a.
Pamoja
na kufanya utambulisho rasmi kwa viongozi hao, Nsekela ambaye
aliambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Ally
Laay na Maofisa wengine, alitumia pia nafasi hiyo kuwaelezea viongozi
hao juu mikakati yake ya kuipeleka mbele zaidi Benki ya CRDB na kuomba
ushirikiano zaidi wa kibiashara kutoka kwa viongozi hao na taasisi
wanazoziongoza.
Kwa
upande wao viongozi hao waandamizi, pamoja na kumpongeza Nsekela kwa
uteuzi huo mkubwa, walimuahidi kumpa ushirikiano na kumhakikishia kuwa
wako tayari kuendelea kuwa wadau wakubwa wa Benki ya CRDB katika
mikakati yake ya kibiashara.
Viongozi
hao pia walipongeza sana jitahada za Benki ya CRDB katika kusaidia
juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, zenye kulenga kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kujenga
Tanzania yenye uchumi wa Kati unaoshamirishwa na viwanda.
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha
ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally
Laay (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid
Nsekela, aliyemtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha,
tangu alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, Kamishna
Diwani Athumani (kulia) akizungumza jambo wakati wa kikao chake na
viongozi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (Mwenyekiti), Abdulmajid Nsekela
(Mkurugenzi Mtendaji) pamoja na Tully Esther Mwambapa (Mkurugenzi wa
Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja) ambao walimtembelea kwa lengo la
kumtambulisha, Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, Kamishna
Diwani Athumani (wa pili kulia) akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa Benki ya CRDB, Ally Laay na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti
na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa.
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers
Siang’a, akizungumza jambo wakati wa kikao chake na viongozi wa Benki ya
CRDB waliomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kumtambulisha Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kushoto).
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers
Siang’a, akifurahi jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki
ya CRDB, Ally Laay (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
CRDB, Abdulmajid Nsekela, baada ya kiko chao, ofisini kwake, jijini Dar
es salaam.
Picha ya pamoja.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kulia), Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia) pamoja na
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa
wakimsikiliza Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully
Esther Mwambapa, alipokuwa akifafanua jambo.
No comments :
Post a Comment