Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya
akiongea na wagonjwa kwenye dirisha la dawa lililopo hospitalini hapo
ambapo wagonjwa walisema wanapata dawa hizo bila malipo
Dkt.Mpoki akimjulia hali mmoja wa
wagonjwa kwenye wodi ya wanaume hospitalini hapo na kuahidi wizara yake
ipo mbioni kusogeza huduma za saratani kwenye baadhi za hospitali za
rufaa za kanda na mkoa ili kuondoa adha ya kusafiri kwenda ocean road.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya
akisisitiza wananchi (hawapo pichani) kuandika maoni na kuweka kwenye
Kisanduku kuhusiana na huduma zinatolewa katika Taasisi ya Saratani ya
Ocean Road ili uongozi uweze kusoma na kuyafanyia kazi maoni hayo.
Katibu
Mkuu akisikiliza wagonjwa waliofika kupata huduma kwenye hospitali
hiyo.Dkt. Mpoki aliutaka Uongozi wa hospitali hiyo kufanyia kazi
malalamiko ya ndugu wa wagonjwa kama mrejesho wa utoaji huduma
……………………………………………………………………
Na.WAMJW, Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya amewataka
Madaktari wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kutimiza wajibu wao
katika kuwahudumia wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kila siku na
kumuagiza Mkurugenzi wa Huduma za Uhakiki na Ubora kutoka Wizarani
kwake kufuatilia.
Dkt.Mpoki ametoa agizo hilo alipotembelea taasisi hiyo ili
kujionea hali ya utoaji huduma pamoja na kusikiliza wagonjwa wanaofika
kupata huduma kwenye taasisi hiyo kutokana na kulalamikiwa kwa baadhi
madaktari na wauguzi “Taasisi hii ni ya faraja lazima mtengeneza
mazingira mazuri yakuwahudumia wagonjwa,kwani ndugu wanafuatilia hali za
wagonjwa wao hivyo jamii inapolalamika tusiseme moja kwa moja ni waongo
bali tushughulikie malalamiko yao ,kama huna jibu muelekeze kwa mtu
ambaye anaweza kumpa jibu ili aweze kupata faraja”.Alisisitiza
Dkt.Mpoki.
Aidha, aliwataka watumishi wa taasisi hiyo kuvaa
vitambulisho ambavyo vinaweka wazi utambulisho wao ili ndugu na wagonjwa
waweze kuwatambua na kutaja ni nani ambaye hajatimiza wajibu wake
ipasavyo.
“watakaoshindwa kwenda nasi tutawapeleka kwingine,hatutaki
maumivu yawe sehemu ya uzoefu wa wagonjwa wanaolazwa Ocean Road,nyinyi
kazi yenu ni kuwahudumia wagonjwa”.
Hata hivyo aliwataka madaktari wabobezi (Mabingwa) kutimiza
wajibu wao na sio kuwaachia jukumu la kuwahudumia wagonjwa madaktari
waliopo mafunzo kwa vitendo”kuanzia sasa tukigundua mgonjwa ameachiwa
daktari wa mafunzo kwa vitendo tutawaondoa wasifanye mazoezi hapa lazima
tuishi kwa kutii na kufuata miiko ya taaluma zetu”alisema dkt.Mpoki
Aliagiza kufanyika mikutano ya ndani mara kwa mara ya
kufuatilia utendaji kazi wa taasisi na kujibu malalamiko yanayotolewa
kwenye mitandao ya kijamii pamoja na masanduku ya maoni ili kupata
mrejesho kutoka kwa wananchi ili kuboresha huduma zinazotolewa kwenye
taasisi.
Kuhusu adha ya umbali wa kufuata huduma kwenye taasisi hiyo
Dkt. Mpoki aliwathibitishia wagonjwa na ndugu waliopo hospitalini hapo
kuwa Serikali kupitia wizara ya afya iko mbioni kupeleka huduma za
saratani kanda ya kusini mara tu itakapokamilika hospitali ya Rufaa ya
kanda,pia huduma kama hizo zipo mbioni kupelekwa kwenye hospitali ya
rufaa ya Tabora pamoja na hospitali maalum ya Benjamin Mkapa iliyopo
jijini Dodoma kwani ni wajibu wao kuhakikisha huduma hizo karibu na
wananchi.
No comments :
Post a Comment