Friday, November 30, 2018

JUMLA YA WATOTO 80 WENYE MATATIZO YA MOYO KUFANYIWA UPASUAJI KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE


Picha 2-min Picha 1-min
Watoto ambao ni wagonjwa wa moyo kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania
wakiwa na wazazi wao wakisubiri kulazwa wodini kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji
wa moyo na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana wenzao wa mradi wa afya wa Little
Hearts wa nchini Saudi Arabia ambao ni moja ya mradi wa Afya ulioko ndani ya

Taasisi ya Msaada ya Muntada yenye makao Makuu yake mjini London nchini
Uingereza. Jumla ya watoto 80 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo
ya matibabu ya siku nane.
…………………..
Na: Genofeva Matemu – JKCI
Jumla ya watoto 80 wenye matatizo ya moyo wanatarajiwa
kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya matibabu
itakayofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mradi wa Little
Heart wa nchini Saud Arabia ambao ni moja ya mradi wa Afya ulioko ndani ya
Taasisi ya Msaada ya Muntada yenye makao Makuu yake mjini Londoni nchini
Uingereza
Matibabu hayo yatahusisha upasuaji wa moyo wa kufungua kifua kwa watoto
wenye matatizo makubwa na upasuaji wa bila kufungua kifua kupitia tundu
dogo kwenye paja kwa watoto wenye matatizo yasiyohitaji upasuaji wa
kufungua kifua.
Watoto wanaotarajiwa kufanyiwa matibabu hayo katika kambi hiyo
wameshafika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kufanyiwa
uchunguzi wa awali tayari kwa kulazwa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji huo.
Kambi hiyo ya siku nane inatarajia kuanza kesho tarehe 1 Desemba 2018 hadi
tarehe 8 Desemba 2018 kwa kutoa matibabu ya kina kwa watoto wote
walioandaliwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya magonjwa ya moyo.
Tangu mwaka 2015 jumla ya watoto 296 wameshafanyiwa upasuaji na
madaktari kutoka mradi wa Little Heart kwa kushirikiana na madaktari
bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa JKCI ambapo watoto 111
walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na watoto 185 walifanyiwa upasuaji
wa bila kufungua kifua.
Hii ni mara ya nne kwa madaktari wa Little Heart wa nchini Saud Arabia
ambao ni moja ya mradi wa Afya ulioko ndani ya Taasisi ya Msaada ya
Muntada yenye makao Makuu yake mjini London nchini Uingereza kuja hapa
nchini kwa ajili ya kutoa matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto kwa
kushirikiana na madaktari wa JKCI.

No comments :

Post a Comment