HakiPensheni
Kamishna wa Mamlaka
ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Kamishna Dkt.Baghayo Saqware
Na Christian Gaya
www.majira.co.tz majira Ijumaa 30 Novemba 2018
Zaidi
ya miaka tisa iliyopita msimamizi wa biashara ya bima nchini (TIRA) amekuwa
akifanya kazi kubwa ya kubadilisha sekta ya bima na kuifanya iweze kukubalika
kwa ujumla mbele ya macho ya umma, akiwa na lengo la kufanya sekta hii kuweza
kuwa na mchango unaoleweka kwenye kipato cha Taifa...
Kwa
jinsi hii kamishana amekuwa akijitahidi kuhakikisha ya kuwa kampuni za bima
zinakuwa na mtaji wa kutosha na watalaamu wanaondesha sekta hii wanafuata utaratibu
na sheria za soko hasa kwenye maeneo ya tozo na madai ya malipo ya bima na
mambo mengine muhimu kwa ukuaji wa biashara ya bima nchini. Hizi juhudi zinaturudisha nyuma
wakati huo wa Kamzola kama Kamishana wa Bima na mpaka sasa kwenye utawala wa Dkt
Sagware Baghayo.
Lakini
pamoja na uchambuzi wa kina wa juhudi hizi ambazo ni baadhi za jitihada za
TIRA, matokeo yanaonesha ya kwamba pamoja na baadhi ya maendeleo katika eneo la
kujituma na kueleweka kwa sekta hii kwa watu kwa miaka ya hivi karibuni, TIRA
na wanaendesha sekta hii bado hawajaanza kuvuna matunda ya juhudi zao
walizotumia na wanazo endelea kutumia kuhamasisha umma juu ya biashara ya bima.
Mojawapo
ya sababu ukweli umebaki pale pale ya kuwa hawa wote akiwemo msimamizi wa
biashara ya bima na waendeshaji wa bima nchini hawafanyi pamoja na kutembea
hatua zile zile zinazofanana katika juhudi zao.
Kwa
kweli idadi kubwa ya watanzania hasa wale walioko vijijini hawana wazo lolote
juu ya bima inashughulika na nini, na faida zake wanazoweza kunufaika nazo kwa
sababu ya ukosefu wa elimu inayohusu bima kwa ujumla.
Kuondoa
tatizo hili labda kamishana wa bima anahitaji kuwa mbunifu sana kwa kuja na
mikakati mbalimbali ya makusudi ya kuwafikia wasiofikika, lengo likiwa ni
kuwaweka watanzania wote wawe kwenye wigo wa bima.
Kwa
sababu changamoto kubwa ya kutoa huduma ya biashara ya bima kwa watanzania
walio wengi ni umbali, wakati kwa upande wa huduma ya benki wameweza kufanikiwa
kutawanyika kwa kuweka matawi yao mpaka sehemu za ndani zaidi, ambapo biashara
ya bima na huduma ya hifadhi ya jamii bado hawajafanya hivyo.
Tumeona
ya kuwa mara nyingi matawi ya kampuni za biashara ya bima zimeshamiri zaidi
kwenye miji mikuu ya biashara kama vile jijini na mijini tena mikoa ile
inayoshamiri vizuri, huu ni ukweli usiofichika.
Matokeo
yake ni kwamba kwa sababu ya mkusanyiko mkubwa wa kampuni za bima uliozidi,
pamoja na watu wao wa masoko na mawakala kwenye miji mikuu na zaidi kulenga na
kukodolea macho tu kwenye biashara za makampuni ya serikali, mahesabu ya
serikali na kwenye sekta ya watu binafsi.
Wakiwa
wanamikakati na juhudi ndogo au bila kuwa na mikakati ya makusudi ya kuendeleza
na kukuza soko la mtu mmoja mmoja ambalo lipo kule vijijini ambalo hawana
habari nalo na kuachwa pweke.
Ambapo
watoa huduma wa biashara ya bima wanaamua kuzunguka na kukata kona nyingi ndani
ya jiji ili kukamata biashara zilizopo na kukuza mapato yatokanayo na
tozo.
Matokeo
yake hii imesababisha kuwepo kwa ushindani hafifu usiokuwa na afya ambao umetoa
mwanya uliopo wa upunguzaji holela wa bei za bidhaa za bima ambao unaweza kuua
sekta ya bima.
Ingawa
tunaaamini kamishna analifanyia kazi jambo hili kwa kutunga sera zake za
mikakati kuhakikisha ya kuwa mafanikio yote yanakuwa imara yaliyofanywa huko
nyuma na ya sasa kwa lengo la kuingia ndani zaidi ili kupanua uwigo wa biashara
ya bima na hasa kupigania ushindani usiofaa wa bei za bidhaa na huduma za
biashara ya bima.
Kulingana
na takwimu zilizotolewa hivi karibuni na kamishana wa bima anasema, kwa mfano
kwa mwaka unaoshia 31 Desemba 2016, sekta ya bima nchini iliongezeka kwa
asilimia 7.0 kutoka shilingi bilioni 618.9 fedha za Kitanzania mpaka kufikia
shilingi bilioni 660.0 za Kitanzania.
Msingi
mdogo wa mtaji wa waendeshaji wa biashara ya bima imebaki kuwa ndiyo sababu ya
kikwazo ya ukuaji wa sekta, wakati sekta ya kibenki yenyewe inaongeza mtaji
mara kwa mara.
Sekta
hii ya biashara ya bima ili ibaki kuwa na ushindani lazima inatakiwa kuendana
na miendano ya biashara zingine zinazofanywa nje ya Tanzania
Kwa
kila biashara, hasa sekta ya huduma, serikali imebaki kuwa ndiye mtumiaji
mkubwa na mteja mkubwa. Kama serikali ikiweza kubadilika kwa ngazi zote juu ya
tabia kuhusiana na biashara ya bima, tozo zitakazo kuwa zimezalishwa toka
serikalini na serikali za mitaa pekee zinaweza kutosheleza kwa kampuni za bima
kujisimamia zenyewe bila matatizo yeyote na kuwa bima za biashara endelevu.
Kwa
kesi hii, serikali inatakiwa kuwa mstari wa mbele kupitisha sheria ya bima ya
lazima ili kuwashawishi wananchi kuitekeleza, serikali iwe tayari kusikiliza ushauri
kutoka TIRA ambaye ndiye mshauri mkuu wa serikali juu ya mambo ya bima.
Mfano
kama TIRA anaweza kuishauri serikali ya kila wizara, idara na wakala zote kila
moja kuanzisha meza yake ya bima ndani ya ofisi zao. Hii ina maana ya kuwa kila
raslimali za mawakala wa serikali yakiwemo magari yao yatakuwa yamekatiwa bima
na watumishi wote wa serikali watakuwa wamekatiwa bima ya kikundi cha bima ya
maisha.
Hii
ina maana ya kuwa kama hawana bima, kitakapotokea kitu chochote kwa mfanyakazi
kama huyo, familia yake hawatalipwa chochote, na tukio lolote juu ya gari la
serikali pamoja na ndege ya rais ikipatwa na ajali, mtu wa tatu atakapohusishwa
kwa kupatwa na ajali kwa kugogwa huyo dereva kama kawaida atachukulia kwa
sababu gari yake ina namba ya Serikali ya Tanzania (SK), hivyo yuko huru
kumgonga mtu yeyote na kuachiwa huru.
No comments :
Post a Comment