Thursday, November 22, 2018

BUNGE LA VIJANA LAENDELEA NA VIKAO VYAKE JIJINI DODOMA


 Spika wa Bunge la Vijana, Mhe. Zephania Sane akiongoza Kikao cha Pili cha Mkutano wa Bunge la Vijana mwaka 2018, mezani wa kwanza mbele ni Katibu wa Bunge hilo,Bi Alphosina Ambrose akiambatana na Makatibu Mezani.Mkutano huo wa Bunge la Vijana unafanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge la Vijana, Mhe. Zephania Sane akiongoza Kikao cha Pili cha Mkutano wa Bunge la Vijana mwaka 2018. Mkutano huo wa Bunge la Vijana unafanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
 Mbunge wa Bunge la Vijana kutokea upande wa Upinzani, Mhe. Julius Mtatiro akiuliza swali Bungeni wakati kikao cha Bunge hilo la Vijana kinachoendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
 Waziri wa Kazi na Ajira katika Bunge la Vijana, Mhe. Victoria Ngowi akijibu  swali la mbunge wakati kikao cha Bunge la Vijana kikiendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
Viongozi mbalimbali wa Upinzani katika Mkutano wa Bunge la Vijana, wa kwanza kushoto ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika bunge hilo, Mhe. Mrisho Juma Ndili, anayefuata ni Waziri Kivuli wa Elimu Mhe. Saidina Hussein na Mhe. Julius Mtatiro.
Mwanasheria Mkuu wa  Serikali katika Bunge la Vijana, Mhe. Shabir Bigirwa akijibu  maswali ya wabunge wakati kikao cha Bunge la Vijana kinachoendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. 
 Wabunge wa Bunge la Vijana mwaka 2018 wakifuatulia mjadala katika Kikao cha Bunge hilo, wa kwanza kushoto katika mstari wa kwanza ni Waziri Mkuu, Mhe. Ally Yanga, anayefuata ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Shabiri Bigirwa na Waziri wa Elimu Mhe. Riziki Bakari.
Baadhi ya wabunge wa Bunge la Vijana mwaka 2018 wakifuatulia mjadala katika Kikao cha Bunge hilo. Mkutano wa Bunge hilo la Vijana mwaka 2018 unaendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

No comments :

Post a Comment