Kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa
serikali ya Mapinduzi Zanzibar na mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa
maendeleo ya jamii Ladislaus Mwamanga (mwenye suti ya rangi ya ugolo) na
baadhi ya viongozi mkoani Pwani na halmashauri ya Kibaha Vijijini,
wakipatiwa maelezo wakati walipotembelea kilimo cha bustani huko
Disunyara Kibaha Vijijini. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Naibu waziri ,ofisi
ya makamu wa pili Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mihayo N’hunga
akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi
wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyofanyika Kibaha Vijijini
Mkoani Pwani. (picha na Mwamvua Mwinyi)
…………………………………………….
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
MKURUGENZI wa mfuko
wa maendeleo ya jamii -TASAF, Ladislaus Mwamanga amesema, bado zipo kaya
maskini 6,048 sawa na asilimia 30 Tanzania Bara na Visiwani, ambazo
hazijafikiwa katika utekelezaji wa mpango kunusuru kaya maskini .
Aidha , wale ambao
wameshanufaika awamu ya kwanza ya mpango huo watafanyiwa tathmini, na
wameandaa mkakati wa kuwapima kwa vigezo vya kuwa na hali nafuu kwa
utaratibu ili watoke na wapishe wengine.
Akiweka bayana juu ya masuala hayo, wakati wa
ziara ya kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya
Mapinduzi Zanzibar iliyofanyika Kibaha Vijijini Mkoani Pwani, alisema
maeneo ambayo hayakufikiwa ,utekelezaji utaanza mwezi april 2019 ,ili
kukamilisha maeneo yote nchi nzima 16,048.#
Mwamanga alisema vijiji,sheia na mitaa 10,000 wameshavifikia hadi sasa .
Alifafanua, kuna
kaya maskini ziliachwa kwenye mpango kwa sababu mbalimbali nao
wataingizwa kwenye mfumo thabiti ili kuwa na rekodi sahihi kwa nchi
nzima.
Hata hivyo ,alisema kaya ambazo zina wazee na wenye ulemavu wataendelea kuwasaidia ili kukidhi mahitaji yao ya msingi.
Akizungumza baada ya
kupokea taarifa hiyo, Naibu waziri ,ofisi ya makamu wa pili Rais wa
serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mihayo N’hunga alisema, serikali ipo
katika hatua za mwisho za kisera kutatua changamoto ya muda mrefu kwa
kaya ambazo hazikujumuishwa katika mpango .
Alifafanua ,kaya
hizo hazikuweza kujumuishwa kutokana na kutofanyiwa dodoso na baadhi ya
walio fanyiwa dodoso kukataa mpango kwa madai kwamba hauna manufaa kwao.
N’hunga alisema, kupitia madodoso hayo ,serikali
ikajumuisha watu hao kwenye mpango kupitia changamoto hizo ,kuboresha
sera na utaratibu uliopo ili kupunguza changamoto hiyo Bara na Visiwani
kwa lengo la kuwafikia watanzania maskini katika ngazi ya sheia,kata,
mitaa na vitongoji .
Hata hivyo alieleza dhamira ya serikali zote
mbili kufikia april 2019 kaya zilizopo kwenye vijiji,sheia na kata
ambazo hazijafikiwa waweze kufikiwa .
Katibu tawala
msaidizi mkoani Pwani ,Abdulrahman Mdimu alisema, wanakabiliwa na
changamoto ya baadhi ya kaya maskini katika vijiji 86 ,mitaa 33
kutofikiwa kutokana na upungufu wa raslimali fedha .
Alitaja changamoto nyingine ni baadhi ya
walengwa kukataa kuingizwa kwenye mpango kwa madai serikali haiwezi
ikatoa fedha bure ,mitazamo hasi wakidhani kuwa kaya ikitambuliwa ni
maskini ni kufedheheka.
Kamati hiyo ilitembelea pia ,mradi wa kutoa
ajira ya muda -uvunaji wa maji ya mvua katika zahanati ya Disunyara kata
ya Kilangalanga na kilimo cha bustani ,ambapo kaimu mratibu TASAF
halmashauri ya Kibaha Vijijini Halima Bira, alisema mpango huo umekuwa
mkombozi katika jamii .
Halima alisema ,mpango huo ulianza kutekelezwa
2012 na jumla ya kaya 7,250 zilitambuliwa na kati ya hizo kaya 5,600
kutoka vijiji 45 ziliandikishwa kwenye mpango.
Shuhuda wa utekelezaji wa mpango wa TASAF ,huko
Disunyara Athumani Shabani alisema,ameweza kusomesha watoto ,wameibua
miradi na wazee wananufaika kupitia mradi huo .
No comments :
Post a Comment