Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akisaliana
na Bibi Aisha Hamisi wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Kiomboi
Wilayani Iramba Mkoani Singida kuangalia hali ya utoaji wa huduma za
Afya, Ustawi na Maendeleo ya Jamii.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Na Mwandishi Wetu Singida
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amemuagiza Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa
Jamii Bw. Rabikira Mushi kuhakikisha Bibi. Aisha Hamisi aliyeishi
zaidi ya miaka kumi katika Hospitali ya Kiomboi iliyopo Wilaya ya Iramba
Mkoani Singida anapelekwa katika Makao ya kuhudumia Wazee na
Wasiojiweza.
Hatua hiyo imekuja baada ya
Naibu Waziri huyo kuongea na Mzee huyo na kupata
taarifa kuwa hana ndugu
wala Jamaa wa kumlea hivyo anakosa huduma muhimu za kibinadamu wakati
wa ziara yake katika Hospitali ya Kiomboi iliyopo Wilaya ya Iramba
Mkoani Singida.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Afisa
Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Iramba amemueleza Naibu Waziri Ndugulile
kuwa Bibi Aisha Hamisi amekaa zaidi ya miaka kumi katika Hospitali ya
Kiomboi alikuwa akitibiwa na kuendelea kukaa hapo kwa kukosa ndugu wa
kumchukua na kumtunza.
Aidha Dkt. Ndugulile ameagiza Mzee huyo apelekwe katika
Makao ya kuwahudumia Wazee na Wasiojiweza ya Sukamahela yaliyopo Wilaya
ya Manyoni ili kupata huduma muhimu.Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Serikali ina jukumu la kuwatunza Wazee na Wasiojiweza kwa wale ambao hawana ndugu wala jamaa wa kuwatunza.
Akipokea maelekezo hayo Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi amesema kuwa suala la kumuhamishia Bibi Aisha kwenye Makao ya Wazee litafanyika mara moja na hatahamishiwa katika Makao ya Wazee ya Sukamahela.
Kwa upande wake Bibi Aisha Hamisi amemshukuru Naibu Waziri kwa kuja kutembelea Hospitali ya Kiomboi na kumwomba kutatua changamoto za matibabu zinazowapata Wazee.
No comments :
Post a Comment