Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama (Mb) akisalimiana na baadhi ya watendaji alipowasili katika
kiwanda cha sukari cha Mkulazi (Mbigili), Mkoani Morogoro kukagua na
kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. William Erio akimwelezea
jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipotembelea kiwanda
cha sukari cha Mkulazi kilichopo Mbigili, Mkoani Morogoro alipofanya
ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda
hicho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama (Mb) akisisitiza jambo kwa watendaji wa kiwanda hicho na
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw.
William Erio alipofanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya mradi
wa ujenzi wa kiwanda hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. William Erio akisisitiza jambo
kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipotembelea mashamba
ya miwa ya kiwanda cha sukari cha Mkulazi kilichopo Mbigili, Mkoani
Morogoro kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda
hicho.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
katika kiwanda cha sukari cha Mkulazi Bw. Gerald Sondo akimuonesha
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) eneo la shamba walilopanda
hekta 860 za miwa ambayo imekwa bila kutegemea umwagiliaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama (Mb) akizungumza na watendaji wa kiwanda cha Sukari cha Mkulazi
kuhakikisha wanatumia mradi huu kuleta manufaa yanayotarajiwa.
Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. William Erio
akifafanua jinsi mtambo wa kuvutia maji ya kisima unakavyokuwa unafanya
kazi ya umwagilia. (Katikati) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
(Mb) alipofanya ziara ya ukaguzi katika
kiwanda hicho.
Na Mwandishi wetu
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama (Mb) ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha
sukari cha Mkulazi (Mbigili) Mkoani Morogoro kujionea maendeleo ya
Ujenzi wa kiwanda hicho kuelekea katika hatua ya kuanza uzalishaji.
Akizungumza
katika ziara hiyo, Waziri Mhagama amewataka watendaji wa Mradi wa Ujenzi
wa kiwanda hicho pamoja na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
kuhakikisha wanatumia mradi huo kwa manufaa ya Taifa na kuwasisitizia
wafanye kazi kwa weledi ili kuendeleza kiwanda hicho wakizingatia
uadilifu katika utendaji kazi wao.
“Lazima kila
mmoja wenu atekeleze majukumu yake kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa
na Serikali ili azma ya kuanzishwa kwa kiwanda hiki itimie, kwa kuwa nia
ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mhe. Rais Dkt John
Magufuli ni kuhakikisha kuwa inajenga uchumi wa viwanda ambao ni
jumuishi na unalenga kuwanufaisha wananchi wote na manufaa ya kiwanda
hiki ni kwa wanachama”. Alisisitiza Mhe Mhagama
Akifafanua Zaidi,
amesema kuwa Kiwanda hicho kitakapoanza uzalishaji kitatoa ajira kwa
watanzania wengi na kuchangia katika kukuza uchumi wa Taifa letu.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw.
William Erio aliahidi kuyafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na Waziri
Mhagama na kumhakikishia kuwa watashirikiana na Bodi ya Wadhamini ya
Shirika hilo kusimamia kwa uadilifu mkubwa mradi huo.
Pia alisisistiza
kuwa wataendelea kufanya juhudi kubwa katika kutekeleza mipango yote
itakayowezesha kuanza mapema iwezekanavyo kwa uzalishaji wa sukari
katika kiwanda hicho.
Ziara hiyo ya
Waziri Mhagama ililenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa kiwanda
cha Sukari cha Mkulazi pamoja na kukagau mashamba ya Miwa ya kiwanda
hicho ili kujionea hatua iliyofikiwa katika kuelekea kwenye uzalishaji
wa sukari na muelekeo wa uchumi wa viwanda nchini.
No comments :
Post a Comment