Wednesday, October 31, 2018

BENKI YA KCB TANZANIA YATOA MSAADA WODI YA WANAWAKE KATIKA HOSPITALI YA RUFAA AMANA


Christine
Mkuu wa Masoko, Mawasililiano na Mahusiano wa Benki ya KCB, Christine Manyenye(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye mkutano wa makabidhiano ya misaada mbalimbali ikiwemo vitanda 10 magodoro 10, mashuka 20, vyenye thamani ya shilling 6,017,000 katika wodi ya wananwake Hospitali ya Amana Ilala Jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dr. Amim Kilomoni.
Dkt. Amim
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali Ya Amana, Dr. Amim Kilomoni akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa makabidhiano ya misaada mbalimbali toka Benki ya KCB ikiwemo vitanda 10 magodoro 10, mashuka 20, vyenye thamani ya shilling 6,017,000 kwa wodi ya wanawake katika Hospitali hiyo leo jijini Dar Es Salaam.
Makabidhiano
Mkuu wa Masoko, Mawasililiano na Mahusiano wa Benki ya KCB, Christine Manyenye (kushoto) akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dkt. Amim Kilomoni moja kati ya Vitanda na Vifaa vingine vyenye thamani ya Tsh 6,017,00/= kwa wodi ya wanawake Hospitali ya Amana, Dar Es Salaam
Picha ya Pamoja
Wafanyakazi wa KCB na Wauguzi wa Hospitali ya Amana wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya Benki ya KCB kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya TSh . 6,017,000 kwa wodi ya wanawake leo kwenye Hospitali ya Amana Ilala, Dar Es Salaam.
Wanahabari
Baadhi ya waandishi waliohudhuria mkutano wa makabidhiano.
………………………………………………………………………………
Benki ya KCB Tanzania imekabidhi msaada wenye thamani ya milioni 6 kwa wodi ya wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa hafla ya  makabidhiano  Mkuu wa Masoko, Mawasililiano na
Mahusiano wa benki hiyo, Christine Manyenye alisema  kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya benki katika uwekezaji  jamii kwa ajili ya kusaidia jamii zilizo na uhitaji.
 
“Benki ya KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya vipaumbele vya Afya, Elimu, Mazingira, Ujasiriamali na masuala ya ubinadamu”, Bi. Manyenye alisema na kubainisha kwamba tangu benki hiyo ilipofungua milango yake hapa Tanzania mwaka 1997, imekuwa ikijikita katika kuisadia jamii.
Benki ya KCB ilikabidhi misaada mbalimbali ikiwemo vitanda 10 magodoro 10, mashuka 20, vyenye thamani ya shilling 6,017,000 katika Hospitali hiyo. Mkurugenzi huyo alisema kuwa upungufu wa vitanda, magodoro na masuka katika hospitali nyingi nchini ni changamoto hasa katika wodi za akina mama na watoto Benki ya KCB iliamua kutoa msaada huo ilikupunguza changamoto hizo.
Akitolea mfano wa michango iliyotolewa na benki hiyo katika kupunguza viwango vya vifo vya kinamama na watoto nchini, Manyenye alisema: “Kupitia miradi hiyo Benki ya KCB Tanzania imeshazisaidia hospitali zaidi ya 15 kwa kuzipatia vifaa tiba mbalimbali.” 
Alizitaja hospitali hizo kuwa ni Muhimbili, Mwananyamala, Ocean Road Cancer Institute, Buguruni, Sinza, Amana, Temeke na Kituo cha Afya cha  Njia (Dar es Salaam); Mt. Meru na Ngarenaro (Arusha); KCMC, St. Thomas na Mawenzi (Moshi); SDA na Makongoro (Mwanza); Hospitali ya Morogoro  (Morogoro); Kivunge Cottage na Kituo cha Huduma za Afya Kombeni  (Zanzibar) na Hospitali ya  Mkuranga (Pwani).
 
Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali Ya Amana, Dr. Amim Kilomoni aliishukuru KCB Bank kwa msaada waliotoa kwani utasaidia kupunguza changamoto zilizokuwa zinawakabili, ikiwamo uhaba wa vitanda, magodoro na mashuka.

No comments :

Post a Comment