Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia chumba
cha kuhifadhia maiti, wakati alipokagua ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya
Mauno Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018, kutoka kushoto ni Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma
Godwin Mkanwa, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dk. Ikaji Rashid. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi
wa Kata ya Mauno wilayani Kondoa, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
alipowasili katika kata hiyo akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Dodoma,
Septemba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza
wananchi wa Kata ya Mauno wilayani Kondoa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi
Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akizungumza na wananchi wa Kata ya Mauno Kondoa Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments :
Post a Comment