Mkuu
wa Utawala na Rasilimali Watu wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na
Kijamii (ESRF), Bw. Deodatus Sagamiko akitoa neno la ukaribisho kwa
niaba ya Mkurugenzi wa ESRF Dk Tausi Kida wakati wa Mkutano wa 5 wa
maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika
ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Mchumi
Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Lorah Basolile Madete
akitoa neno la ufunguzi wakati wa Mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa
miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa
Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
Mratibu
wa Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab)
kutoka ESRF, Mussa Martine akizungumza na waandishi wa habari wakati wa
mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni
mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na
Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
Bw.
Anton Cartwright wa Kituo cha Afrika cha miji kutoka nchini Afrika
Kusini akiwasilisha Muhtasari wa tafiti tatu zilizofanyika chini ya
Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab) na
kuongoza majadiliano kuhusu athari za kisera katika tathmini ya kitaifa
ya mabadiliko kuelekea miji (National Urbanization Transition Assessment
-NUTA) wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania
uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya
Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
Yash
Ramkolowan wa DNA Economics kutoka Afrika Kusini akiwasilisha Utafiti
wa kuoanisha athari za kiuchumi kwa kuangalia njia mbili zinazotumika
Tanzania kuelekea uchumi wa kati wa viwanda wakati wa mkutano wa 5 wa
maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika
ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF),
jijini Dar es Salaam.
Gemma
Todd kutoka Ifakara Health Institute (IHI), akiwasilisha matokeo ya
awali ya utafiti wa mipango miji wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya
ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa
mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar
es Salaam.
Mratibu
wa Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab)
kutoka ESRF, Reshian W. Kanyatila akielezea masharti ya ushiriki katika
shindano la utoaji huduma katika majiji.
Mtafiti
Msaidizi na Mratibu wa Miradi wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Bw. Emmanuel
Njavike (katikati) akiwasilisha waliyojadili katika kikundi kazi wakati
wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya washiriki wakitoa maoni wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji
wa miji Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya
Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wataalam walioshiriki mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji
Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti wa
Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jana jijini Dar es Salaam.
Mchumi
Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Lorah Basolile Madete
(kushoto), Mshehereshaji wa mkutano ambaye pia ni Mtafiti Mshiriki wa
ESRF, Dr. Jane Mpapalike (katikati) pamoja na Bw. Anton Cartwright wa
Kituo cha Afrika cha miji kutoka nchini Afrika Kusini wakijadiliana
jambo wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania
uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya
Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
Msanii
wa Bongo Flava, Beka Flava akitoa burudani ya wimbo maalum wakati wa
mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni
mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na
Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja
Na Mwandishi wetu
IMEELEZWA
kuwa katika mazingira ya sasa ya kuipeleka Tanzania katika uchumi wa
kati kwa kuwa na viwanda ni lazima taifa litakuwa na mabadiliko katika
makazi na kwamba miji mingi itachipuka.
Aidha
serikali inapotekeleza mpango wake wa pili wa maendeleo
2016/17-2020/21 katika mpango wa muda mrefu wa maendeleo kwa lengo la
kuwezesha mabadiliko ya kiuchumi kwa maendeleo ya watu uwepo wa miji ni
wa lazima.
Aidha
mazingira duni ya maisha katika vijiji kunafanya watu kuhamia katika
maeneo yenye shughuli mbalimbali na hivyo kukuza miji iliyopo.
Hayo
yalisemwa na Dk Lorah Basolile Madete, Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara
ya Fedha kwenye mkutano wa mkutano wa 5 wa jukwaa la ukuaji wa miji
Tanzania (Tanzania Urbanisation Laboratory – TULab) ulioambatana na
uwasilishaji wa tafiti tatu zilizofanywa na TUlab kuanzia mwaka jana.
Pia
alisema tofauti kubwa ya kipato iliyopo vijijini na mijini inafanya
maeneo ya jirani na vijiji kubadilika na kuanza kuchukua muonekano wa
miji.
“Ndio
kusema ni lazima kujiandaa kwa mabadiliko hayo na kuwa na mpangilio wa
kudhibiti ukuaji wa miji, kinyume chake Tanzania haitaweza kuvuna faida
katika uchumi, kijamii na kimazingira kama miji itakua ghafla bila
mipango mathubuti” alisema Dk Madete.
Katika
mkutano huo ilielezwa kuwa kudhibiti miji ni kitu muhimu ikiwa mataifa
yanataka kuwa na maendeleo endelevu ya kiuchumi na ustawi wa jamii.
Miji
hiyo inatakiwa kupangwa na kukua kwa mujibu wa makubaliano ya dunia
kama yale ya Paris na maendeleo endelevu yaliyokubaliwa na Umoja wa
Mataifa.
Pia
makubaliano mengine yanayotakiwa kuzingatiwa ni New Urban Agenda,
Ajenda ya maendeleo ya Afrika ya 2063, Mikataba ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki na ule wa Ushirikiano wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Kwa
kutekeleza makubaliano hayo Tanzania itakuwa inajiweka sawa katika
uendelezaji wa miji yake katika hali ambayo inaleta tija na kuongeza
ufanisi kwa yale yanayofanyika katika mji.
Katika
mpango wa pili wa Maendeleo serikali ya Tanzania imesema wazi kwamba
inakuwa na miji iliyopangwa na inayotoa huduma kwa ufanisi kama ya
utunzaji wa mazingira, uondoaji wa taka na maji taka, mambo ya
usafirishaji na nishati safi ya kuaminika.
Hata
hivyo imeelezwa kuwa kazi ya kuendeleza miji haiwezi kufanywa na
serikali pekee bali na wadau wengine ambao wanatambua thamani ya
upangaji miji.
Katika
suala la ushirikiano ndilo linafanya uwepo wa Jukwaa la Ukuaji wa Miji
Tanzania (TULab) kuwa la muhimu ili kuwa na uhakika wa maendeleo ya miji
kwa kuisaidia Serikali kufanya maamuzi yenye uhakika na tija.
TULab
ilianzishwa Agosti 2017 na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na ESRF na
Coalition for Urban Transitions (CUT) na kufanya tafiti tatu
zilizowasilishwa na Bw. Anton Cartwright wa Kituo cha Afrika cha Miji,
Afrika Kusini.
Bw.
Anton aliwasilisha Muhtasari wa tafiti tatu zilizofanyika chini ya
Jukwaa hilo linaloshughulikia mabadiliko kuelekea miji bora Tanzania au
kwa ufupi TULab na jinsi tafiti hizo zitakavyosaidia kuandaa mwongozo
wa ukuaji bora wa miji Tanzania (National Urbanisation Roadmap).
Naye
Bw. Yash Ramkolowan kutoka Afrika Kusini aliwasilisha Utafiti utakao
angalia uhusiano kati ya viwanda na ukuaji wa miji Tanzania huku Gemma
Todd kutoka Ifakara Health Institute (IHI) aliwasilisha matokeo ya awali
ya utafiti wa mipango miji.
Naye
Mratibu wa TULab. Reshian W. Kanyatila, alizungumzia Shindano la Utoaji
Huduma Bunifu zitakazosaidia kuboresha Jiji la Dar es salaam na
masharti ya jinsi ya kushiriki katika shindano hilo.
Awali
akifungua mkutano kwa niaba ya Mkurugenzi wa ESRF Bw. Deodatus Sagamiko
alisema kwamba tangu mwaka jana kuanzishwa kwa TUlab, tafiti tatu
zimefanyika ambazo zinafungua ukurasa wa kuanza uandaaji wa mwongozo wa
ukuaji bora wa miji Tanzania. Bw. Deodatus Sagamiko, Mkuu wa Utawala na
Raslimali Watu wa ESRF, alielezea umuhimu wa tafiti hizo na haja ya
kuongeza utafiti mwingine ili kukamilisha maandalizi ya mwongozo huo.
Kutokana
na hatua iliyofikiwa TULab inafanya utafiti unaohusisha maendeleo ya
viwanda na ukuaji wa miji. Pia TULab inaangalia uwezekano wa kuendesha
shindano la ubunifu katika utoaji huduma kwa jiji la Dar es Salaam kabla
mwongozo wa ukuaji bora wa miji kuzinduliwa hapo mwakani.
No comments :
Post a Comment