Thursday, September 20, 2018

VIDEO:Serikali Yafuta Baadhi Ya Tozo Za Kikanuni Zilizokuwa Zikitozwa Na OSHA


????????????????????????????????????
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika katika kujenga uchumi wa viwanda ikiwemo kufuta baadhi ya tozo zilizokuwa zikitozwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) ikiwemo ada ya Leseni ya kukidhi matakwa ya Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi hii leo Jijini Dodoma Septemba 20, 2018.
Pic 2
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) Bi. Hadija Mwenda akizungumzia umuhimu wa kulinda afya na Usalama  kwa wafanyakazi katika maeneo ya kazi wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) na waandishi wa habari  leo Jijini Dodoma.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Kitengo Cha Sheria kutoka Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) Bi. Joyce Mwambungu akifafanua kwa waandishi wa habari juu ya baadhi ya Tozo za kikanuni ambazo zimefutwa kwa mujibu wa Sheria. (Kushoto) ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) Bi. Hadija Mwenda na Mkurugenzi wa Usalama na Afya (OSHA) Bw. Alex Ngata.
????????????????????????????????????
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokutana nao hii leo kuzungumzia hatua zilizochukuliwa na Serikali katika katika kujenga uchumi wa viwanda ikiwemo kufuta baadhi ya tozo zilizokuwa zikitozwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) leo Jijini Dodoma.
????????????????????????????????????
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokutana nao hii leo kuzungumzia hatua zilizochukuliwa na Serikali katika katika kujenga uchumi wa viwanda ikiwemo kufuta baadhi ya tozo zilizokuwa zikitozwa na Wakala wa
Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA).
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
……………….
Na.Alex Sonna wa Fullshangweblog,Dodoma
Serikali imeamua kufuata baadhi ya Ada na Tozo mbalimbali zisizoondoa wajibu kutoka kwa muajiri kwa ajili ya kulinda Afya za Wafanyakazi ili kuweza kuvutia na kuchochea Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda kwa lengo la kuimarisha Maendeleo nchini   .
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma Wazari wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,Vijana na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama amesema kuwa mabadiliko hayo yalifanywa kutoka katika Mamlaka ya Usalama na Afya inayohusiana na OSHA kwa Lengo la kuchangia na kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano kuyaweka mazingira salama kwa wawekezaji.
”Tumeamua kufuta baadhi ya Ada zikiwemo Ada ya kuchukua fomu ya Usajili ambayo gharama yake ilikuwa shilingi 2000 pamoja na Ada ya usajili wa maeneo ya kazi kwa kuzingatia ukubwa wa Eneo ambayo nayo ilikuwa gharama zake ni shilingi 50,000,80o,000 hadi 1,000,000 kwa sasa maeneo hayo ni bure” amesema Mhe.Mhagama
Pamoja na hayo Waziri Mhagama,amesema kuwa wameamua pia kufuta Ada ya Leseni ya kukidhi matakwa ya Sheria ya Usalama na Afya Mahala Pa Kazi ambayo pia ilikuwa ikitozwa kwa Gharama ya shilingi 200,000 kwa mwaka kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha mazingira ya kufanyia biashara kwa sasa leseni hiyo nayo ni bure.
Kwa Upande Wake Joyce Mwambungu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Katika Afya Salama,amesema kuwa OSHA kwa sasa imewekeza nguvu za kutoa Elimu kwa wadau kuhusu tamko la Kisheria la kulinda Afya za Wafanyakazi nchini Mahala Pa Kazi katika Sekta mbalimbali ili kuweza kusimamia mifumo ya Utendaji wa watumishi ili kuondoa Mianya ya Rushwa ili kufanikisha uwazi na uwajibikaji
”Sisi jukumu kubwa zaidi ni kutoa mafuzo na Elimu kwa jamiii ili iweze kujua na kujifunza kwa kupitia Elimu kwa wadau wote nchini ili Takwa hili la kisheria liweze kufanikiwa kwa Kulinda Afya za Wafanyakazi nchi Mahala Pa Kazi na OSHA ipo tayari kuhakikisha uchumi wa viwanda unakuwa na kuleta tija kwa Taifa Letu”amesema Mwambungi

No comments :

Post a Comment