Kassim Majaliwa akifungua Mkutano
Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) kwenye ukumbi wa Jakaya
Mrisho Kikwete jijini Dodoma Septemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Kassim Majaliwa akifungua Mkutano
Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) kwenye ukumbi wa Jakaya
Mrisho Kikwete jijini Dodoma Septemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Kassim Majaliwa akifungua Mkutano
Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) kwenye ukumbi wa Jakaya
Mrisho Kikwete jijini Dodoma Septemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Kassim Majaliwa akifungua Mkutano
Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) kwenye ukumbi wa Jakaya
Mrisho Kikwete jijini Dodoma Septemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi wakati
alipowasili kwenye ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete kufungua Mkutano wa
34, wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa, Septemba 27, 2018. Kulia ni Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa, Selemani
Jafo na kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt, Mary Mwanjelwa. Watatu
kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, Josephat Kandege na watatu kulia ni Meya wa jiji la
Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipata maelezo kuhusu mitambo ya umeme kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Tekinolojia na Masoko wa REA, Elineema Mkumbo (wapili
kushoto) wakati alipotembelea banda la maonyesho la REA kabla ya
kufungua Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Kwenye ukumbi
wa Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dodoma, Septemba 27, 2018. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa Mkutano
Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Mkutano huo kwenye ukumbi wa
Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dodoma, Septemba 27, 2018. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiagana na baadhi ya viongozi walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa 34
wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) Kwenye ukumbi wa Jakaya Mrisho
Kikwete jijini Dodoma Septemba 27, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa ALAT,
Gulaam Hafeez ‘Mukadam’, wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt.
Bilinith Mahenge na wanne kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary
Mwanjelwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
SERIKALI KWA SASA INABORESHA MAENEO YA UTAWALA-MAJALIWA
*Asema lengo ni kuziwezesha halmashauri kujiendesha zenyewe
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema
kipaumbele cha Serikali ya Awamu ya Tano kwa sasa ni kuboresha maeneo
ya utawala kwa lengo la kutekeleza miradi ya maendeleo na
kuongeza uwezo
wa halmashauri kujiendesha zenyewe.
Ameyasema hayo leo (Alhamisi,
Septemba 27, 2018) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya
Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.
Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete, jijini
Dodoma.
Ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo
kwa maombi mengi ya kuanzisha maeneo mapya ya utawala nchini. “Kama
mnakumbuka nimekuwa nikieleza mara kadhaa kwamba tunazishukuru Serikali
za Awamu zilizotangulia kwa kuainisha maeneo ya utawala.”
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema
viongozi hao wanapaswa wajitathmini sambamba na kuainisha mikakati
mizuri ili kuhakikisha lengo la kusogeza huduma kwa wananchi linatimia.
Waziri Mkuu amesema katika kipindi
cha mwaka 2014/15 jumla ya halmashauri 66 na mkoa mmoja wa Songwe
vilianzishwa pamoja na vijiji 1,949, mitaa 1,379 na vitongoji 8,777.
Hadi sasa, maeneo hayo hayajaweza kuwa na miundombinu, vifaa na
watumishi wa kutosha ili kuwezesha wananchi kupata huduma
iliyokusudiwa.
“Mathalani, mkoa wa Songwe
halmashauri zake zote, hata halmashauri ya wilaya ya Mbozi ambapo ndiyo
makao makuu ya mkoa bado haujafikia vigezo vya kuwa Manispaa. Baadhi ya
halmashauri zinaendelea na ujenzi wa ofisi wakati nyingine kama Mafia,
Rufiji, Handeni na Ludewa zipo kwenye magofu na huwezi kuamini kama ni
Ofisi za Halmashauri.”
“Taarifa nilizonazo hadi sasa ni
kwamba tayari sh. bilioni 120.7 zimepokelewa kwenye halmashauri
mbalimbali kati ya sh. bilioni 238.8 zinazohitajika kukamilisha ujenzi
wa majengo ya halmashauri sawa na asilimia 50.54 ya fedha zote.
Amesema kiasi kilichobaki
kitaendelea kutolewa kupitia bajeti ya Serikali na mapato ya ndani ya
halmashauri, ambapo baadhi yake zitapewa fedha za kukamilisha ujenzi
baada ya uhakiki kwa sababu zimekuwa zikipokea fedha kwa muda mrefu.
Kadhalika, Waziri Mkuu amewaagiza
viongozi wa halmashauri hizo wahakikishe wanajenga Ofisi za Serikali za
Vijiji, Mitaa na Vitongoji badala ya kuendelea kuanzisha Serikali hizo
huku zikiwa hazina hata ofisi.
Kuhusu uhaba wa watumishi wa kada
mbalimbali katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Waziri Mkuu amesema
Serikali inaendelea na zoezi la kuajiri watumishi hususan wa kada za
afya na elimu, ambapo kati ya mwaka 2015/2016 hadi 2017/2018 Serikali
imeajiri watumishi wa kada ya elimu 13,472 na afya 8,238 kwa lengo la
kuziba mapengo yaliyopo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
- L. P. 980,
41193 – Dodoma
ALHAMISI, SEPTEMBA 17, 2018.
No comments :
Post a Comment