Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince
William (wapili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary
Senyamule (watatu kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Uhifadhi wa Faru, Dkt.
Bernad Mchomvu (wakwanza kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA,
Dkt.Allan Kijazi, wakifurahia jambo kwenye hema maalum lililojengwa kama
makazi ya muda ya Mjukuu huyo wa Malkia kwenye hifadhi ya taifa
Mkoamazi Wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro.
NA
K-VIS BLOG, MKOMAZI SAME
MJUKUU
wa Malkia wa Uingereza Prince William, ametumia siku mbili kati ya tatu
alizotembelea nchini Tanzania kupumzika Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro. Prince
William ambaye aliwasili nchini Septemba 23 alilala Dar es Salaam kwa siku hiyo
moja, na kisha baada ya kumaliza ziara yake jijini Dar es Salaam, kwa kukutana
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, na kisha
kutembeela bandari ya Dar es Salaam kabla ya kuelekea Wizara ya Maliasili na
Utalii kwenye ofisi zake ndogo za Dar es Salaam, Prince William aliamua kufanya
mapunziko yake binafsi eneo la Mkoamazi, Wilayani Same.
Siku
hizo mbili alizotumia Mjukuuwa Mfalme kupumzika kwenye eneo la hifadhi ya Mkomazi
inaelezwa kuhamasisha na kuitangaza hifadhi hiyo kimataifa kuwa kati ya hifadhi
zenye mvuto mkubwa Afrika Ziara
ya Prince William barani Afrika, ilianzia nchini Namibia, Tanzania na kisha
Kenya, ililenga kuangalia juhudi za serikali za Afrika katika kukabiliana na
ujangili na biashara ya haramu ya wanayamapori, ili hatimaye atoe ripoti kwenye
mkutano mkubwa wa kidunia utakaofanyika baadaye jijini Lon don Uingereza kujadili
namna ya kuzuia biashara haramu ya wanyamapori duniani. Aidha
akiwa wilayani Same, Prince William alipokea taarifa ya uongozi wa Wilaya hiyo
katika mapambano ya kuzuia biashara haramu ya wanyama pori na hivyo kuonyesha dhamira
ya kusaidia mapambano dhidi ya ujangili. Pia aliahidi kushiriki ukuzaji wa
utalii kwa mipango ya Wilaya na TANAPA. Mjukuu
huyo wa Mfalme aliwaachia ujumbe viongozi wa Wilaya na Watanzania kwa ujumla
ikiwemo TANAPA, kuhakikisha utalii unahusisha wananchi wanaozunguka hifadhi. kwa
kuzingatia utekelezaji wa mipango mikubwa ya kuiboresha inayoendelea. Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule aeleza ukamilishaji
wa mpango mkakati ya kukuza utalii Wilayani utakao unganisha utalii wa hifadhi
ya taifa ya Mkomazi, Mlima Shengena, msitu wa Chome pamoja na utalii wa asili/
utamaduni. Pia
alimueleza fursa za uwekezaji zilizopo wilayani humo ikiwa ni pamoja na
kumkaribisha kuwekeza. Naye
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Dr. Allan Kijazi amueleza juu ya hifadhi za TANAPA na
uhitaji wa kuongeza nguvu ya kupambana na ujangili na kumualika aje tena nchini
kutembelea mbuga nyingine.
Prince
William akitambulishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro
baada ya kutua kwenye hifadhi ya taifa ya Mkomazi wilayani humo.
Prince William akisali miana na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Allan Kijazi
No comments :
Post a Comment