Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia), akikabidhi zawadi ya
pikipiki kwa mmoja wa washindi wa kampeni ya miezi mitatu ya mauzo
iliyopewa jina la 'Mimi ni Shujaa' kwa Patrick Paul jijini Dar es Salaam
hivi karibuni. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa wafanyakazi wa benki hiyo
ina lengo la kuhamasisha utendaji kwa wafanyakazi wanohusika katika
kitengo cha mauzo ndani ya benki hiyo. Wanaoangalia kutoka wa pili
kushoto ni, Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Andrew Lyimo, na
Ofisa Mwandamizi katika Idara ya Wateja Binafasi wa Absa Group, Nazim Mahmood.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Andrew Lyimo, akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi zawadi wafanyakazi bora wa kampeni ya mauzo iliyopewa jina la ‘Mimi ni Shujaa’ ya benki hiyo hivi karibuni.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa tatu kushoto, mstari wa
mbele), akipiga picha ya pampoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’I Issa (kulia kwake)
wakati mkurugenzi huyo pamoja na ujumbe wake wakimtembelea ofisini kwake
na kuzungumzia fursa mbalimbali za ushirikiano jijini Dar es Salaam
hivi karibuni.
No comments :
Post a Comment