TAARIFA KWA MADAKTARI NCHINI
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha watanzania kuwa kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Al-Balsam la nchini Saudi Arabia itakuwa
na kambi maalum ya matibabu ya kusaidia wagonjwa wa moyo ambao mishipa
yao ya damu haipitishi damu vizuri na inahitaji kuzibuliwa kwa kuwekewa
kifaa kiitwacho Stent.
Taasisi
inawaomba madaktari wote wa Hospitali za Rufaa nchini kuwaleta wagonjwa
wenye matatizo hayo ili waweze kufanyiwa matibabu. Wagonjwa wafike
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
tarehe 26/09/2018 kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu
ambayo yataanza tarehe 29/09/2018 hadi tarehe 05/10/2018.
Kwa mawasiliano zaidi piga namba
zifuatazo: 022-2151379,0782-042019,0713-236502,0713-607183,0754-870969
na 0788-465169 ili uelekezwe utaratibu wa kuwatuma wagonjwa hao.
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
19/09/2018
No comments :
Post a Comment