Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta binafsi na Umma, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Dkt.
John Mboya, akizungumzia faida za miradi
ya ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati
za Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na Kamati ya Uwekezaji Mitaji ya umma,
iliyofanyika Jijini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Mashimba Ndaki.
Na
Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
WAJUMBE
wa Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na Kamati ya Uwekezaji na
Mitaji, wameishauri Serikali kutekeleza kwa vitendo miradi mikubwa na yenye
tija kwa Umma kwa kutumia njia ya Ubia kati ya Umma na Sekta binafsi ili
kuchochea haraka maendeleo ya nchi.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Mashimba Ndaki amesema
kuwa wabunge wameridhishwa na na hatua
zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa mpango wa ubia kati ya
Serikali na sekta binafsi unafanikiwa na unachochea maendeleo ya wananchi.
“Kama
wabunge tungependa kuona mpango unaingizwa katika mipango ya Serikali ili
kuharakisha miradi ya maendeleo na pia tunapongeza hatua zilizochukuliwa na
Serikali ikiwemo kumteua Kamishna anayeshughulikia miradi ya ubia kati ya sekta
binafsi na ile ya umma, “ Alisisitiza Mboya
Alibainisha
kuwa jukumu la Serikali ni kuhakikisha kuwa inaweka mazingira wezeshi kwa
wawekezaji wote watakaojitokeza kushirikiana na Serikali katika kutekeleza
miradi ya maendeleo hapa nchini.
Mwenyekiti
wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Mhe. Endrew Chenge amesema kuwa nchi
nyingi Duniani zimefanikiwa kuwaletea wananchi wake maendeleo kupitia utaratibu
huo ambapo jambo la muhimu ni kufanywa kwa maandalizi ya kina na kuwepo kwa
utashi kutasaidia kufanikiwa kwa miradi husika .
Aliongeza
kuwa mwaka huu Serikali imeleta Bungeni Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya PPP
utakaojadiliwa na wabunge katika Bunge linaloanza Septemba 4 mwaka huu, pamoja
na mambno mengine Muswada huo unapendekeza kuanzishwa kwa Kituo cha PPP chini
ya Wizara ya Fedha na Mipango, ambacho kitakuwa na jukumu la kuishauri Serikali
kuhusu masuala yanayo husu miradi mbalimbali itakayowasilishwa kwa mfumo wa
Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi
Akizungumza
katika Semina hiyo, Kamishna wa Ubia
kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. John
Mboya amesema kuwa Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inaweka mazingira
wezeshi katika kutekeleza miradi ya ubia na Sekta binafsi ili kuleta mageuzi
katika maisha ya wananchi.
“Lengo
la kuwa na miradi ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi ni kutekelezaIilani
ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kutekeleza mpango wa maendeleo na hatimaye kutoa
huduma bora kwa wananchi,” Alisisitiza Mboya
Akifafanua
Mboya amesema kuwa moja ya hatua za maboresho zilizochukuliwa na Serikali ni
kuhamisha Kituo cha kusimamia miradi ya ubia katika ya Umma na Sekta binafsi
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuja Wizara ya Fedha.
Akizungumzia
majukumu ya chombo cha kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo Dkt. Mboya amesema kuwa chombo hicho kimepewa jukumu la
kufanya uchambuzi wa kina kuhusu miradi yenye sifa na kusimamia mchakato wa
uteklezaji wa mpango huo kwa kufuata ngazi zote zilizopo hadi utekelezaji wa
mradi husika.
Aliongeza
kuwa ili kufanikisha mpango huo Serikali inasisistiza uwazi, uwajibikaji na
utayari hali itakayo sababisha kufikiwa
kwa malengo ya miradi ya ubia kati ya sekta hizo mbili ambapo alitaja baadhi ya
miradi itakayotekelezwa ambayo upembuzi yakinifu umekamilika kuwa ni ile ya
ujenzi wa Viwanda vya dawa, usambazaji wa gesi majumbani katika Jiji la Dar es
Salaam, Mtwara , Lindi na ule wa uendeshaji wa mabasi ya mwendo kasi Jijini Dar
es Salaam ambao umeanza na uko katika hatua mbalimbali za uendelezwaji.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu
amesema kuwa tayari Bohari hiyo imekamilisha upembuzi yakinifu wa mradi wa
ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba vinavyotokana na malighafi
zinazozalishwa hapa nchini ikiwemo pamba na kufikia machi mwakani zabuni ya
mradi huo itatangazwa ili kuwapata wabia.
Katika
kutekeleza mradi huo kiwanda cha kuzalisha maji ya dripu yanayotumika kwa
wagonjwa mahosipitalini pia kitajengwa ambapo kwa sasa maji hayo yanaagizwa kutoka
nchini Uganda na kwamba hatua hiyo itapunguza gharama za Serikali za kuagiza
dawa na vifaa hivyo kutoka nje ya nchi ambapo zaidi ya shilingi trilioni 1.8 hutumika kuagiza bidhaa hizo kila mwaka.
Kwa
upande wake. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya
Petroli (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba amesema kuwa mradi wa kusambaza gesi
majumbani katika Jiji la Dar es Salaam, Mtwara na Lindi unaotarajiwa kuhgaribu
zaidi ya shilingi bilioni 300, utaleta mageuzi kwa wananchi wa mikoa hiyo
ambapo wananchi zaidi ya 120,000 katika Jiji la Dar es Salaam watafikiwa.
Aliongeza kuwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara wananchi
zaidi ya 5,000 wataunganishiwa gesi majumbani mwao huku viwanda zaidi 30 katika
maeneo ya mradi vitaunganishiwa huduma hiyo pamoja na vituo vya kujaza gesi
kwenye magari yanayotumia nishati hiyo.
Semina
kwa wabunge wa Kamati za Bajeti, Miundombinu na ile ya Uwekezaji Mitaji imefanyika
Jijini Dodoma ikiwashirikisha wajumbe wa Kamati hizo ili kuwajengea uwezo wa
namna dhana hiyo inavyoweza kuleta maendeleo hapa nchini.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati
za kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na
Uwekezaji na Mitaji ya Umma wakifuatilia semina kuhusu dhana ya
utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa njia ya ubia kati ya sekta binafsi na
umma (PPP), Jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), akizungumzia matarajio
ya wabunge katika utekelezaji wa miradi ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi
katika kuchochea maendeleo, wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za
Bunge za Miundombinu, Bajeti na kamati ya Uwekezaji Mitaji ya Umma, iliyofanyika
Jijini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati
za kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na
Uwekezaji na Mitaji ya Umma wakifuatilia semina kuhusu dhana ya
utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa njia ya ubia kati ya sekta binafsi na
umma (PPP), Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge na
Mbunge wa Bariadi Mhe. Andrew Chenge (kulia) na Mbunge wa Ileje Mhe. Dkt.
Janeth Mbene, wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizotolewa na wataalam
kutoka Benki ya Dunia kuhusu masuala ya utekelezaji wa Miradi ya Ubia kati ya
Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Jijini Dodoma.
Wataalamu washauri wa
masuala ya Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (PPP) Bw. Abhijit
Bhaumik (kushoto), Bw. Philip Kelly (katikati)
na Bw. Craig Sugden, wakijadiliana jambo wakati wa semina ya Kamati tatu za
Bunge za Bajeti, Miundombinu na Uwekezaji Mitaji ya Umma, iliyofanyika Jijini
Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu
ya Dawa (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu, akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati za
Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na Kamati ya Uwekezaji Mitaji ya Umma,
ilifanyika Jijini Dodoma kuhusu hatua zilizochukuliwa na taasisi hiyo za
kupanga kujenga viwanda vitatu vya dawa na vifaa tiba kwa kuishirikisha Sekta
Binafsi (PPP).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Mhandisi
Kapuulya Musomba, akiwasilisha
mada kwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za
Bunge za Miundombinu, Bajeti na Kamati ya Uwekezaji Mitaji ya Umma, Jijini
Dodoma, kuhusu hatua zilizochukuliwa na Shirika hilo kutaka kuishirikisha Sekta
Binafsi kutekeleza mradi mkubwa wa kuunganisha gesi majumbani katika katika
mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara kupitia ubia kati na sekta binafsi na
Umma (PPP) utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 300.(PICHA NA WFM)
No comments :
Post a Comment