Saturday, August 25, 2018

WAZIRI UMMY AKABIDHI MADAWATI SHULE YA SEKONDARI TOLEDO TANGA,ATOA NENO KWA WAZAZI NCHINI

IMG_3045
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Toledo mara baada ya kuwakabidhi madawati 40
NA MWANDISHI WEYTU
WAZAZI kote nchini wametakiwa kuacha kulalamikia wadau wa elimu na badala yake wameshauriwa kushirikiana na walimu kukagua madaftari ya watoto wao kwa lengo la kuongeza ufaulu ili kupunguza mimba za utotoni zinazosababisha ndoto zao kushindwa kufikiwa. 
Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati halfa ya kukabidhiano ya madawati na viti vyake 40 aliyoyatoa kwenye shule ya Sekondari Toledo ya Jijini Tanga. 
Ummy ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama cha Mapinduzi {CCM) mkoa wa Tanga alisema kimsingi wazazi wanapaswa kutambua kufanya hivyo kutawasaidia kuwawezesha vijana wao kuongeza ufaulu na hivyo kufanikiwa kuepukana na vishawishi ambavyo wanakabiliana navyo wakati wakiwa shuleni. 
“Ndugu zangu wazazi na walezi lazima tutambue jukumu letu la kufuatilia maendeleo ya watoto wetu kwani hii ndio njia pekee inayoweza kuwasaidia kwa kushirikiana na walimu wao kwa lengo la kuwezesha kufikia ndoto zao”Alisema. Naye ka upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa aliwataka wanafunzi kutumia fursa hiyo kuongeza jitihada kwenye kusoma ili azma ya serikali ya kuongeza ufaulu kwa shule zake iweze kufikiwa. 
“Ndugu zangu wanafunzi mmepata madawati haya yatumieni vizuri kwenye matumizi yaliyokusudiwa kwa lengo la kuwawezesha kufikia malengo yenu kwa kuongeza ufaulu “Alisema. Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Toledo Daudi Nchia alimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo na kuongeza kuwa bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa matundu ya vyoo vya wasichana . 
Alisema kutokana na uhaba huo umesababisha wasichana na wavulana kushiriki katika huduma hiyo.
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM) kulia akimkabidhi madawati 40 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Toledo ya Jijini Tanga Daudi Nchia ikiwa ni mkakati wake wa kukabiliana na uhaba uliopo
IMG_3025 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM) kushoto akiwa amekaa kwenye moja ya madawati 40 aliyokabidhi kwa shule ya Sekondari Toledo Jijini Tanga 
IMG_3048-1 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM) katika akiwa na Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Toledo Daudi Nchia mara baada ya kuwakabidhi madawati 40

MTEKETA: NIMEFIKA DARAJA LA JPM KABLA SIJAFA


 
NA MWANDISNHI MAALUM-KILOMBERO
MBUNGE wa zamani wa Kilombero, Abdul Mteketa (CCM), ametimiza azma yake ya kutembelea daraja jipya la Magufuli lililopo Wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Akizungumza leo baada ya kutembelea daraja hilo, alisema yeye alikuwa ni moja ya viongozi waliopigania ujenzi wa daraja hilo ukamilike haraka wakati Rais Dk. John Magufuli alipokuwa Waziri wa Ujenzi katika Serikali ya awamu ya tatu.
“Kama unavyojua katika maisha yangu ya kuumwa pengine nisingeliona hili daraja. Lakini leo nimefika na kuona kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli.
“Watu wa Kilombero, Ulanga na Malinyi tunamshukuru kwa dhati kiongozi wetu mpendwa ambaye amekuwa akifanya kazi kubwa y
“…tayari umekamilisha ujenzi wa daraja na ameshaweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara kutoka Kidatu hadi Ifaraka- Ulanga, sasa ametufuta machozi watu wa Kilombero-Ulanga na kwa dhati ninampongeza Rais Magufuli,” alisema Mteketa
Akizungumza hali yake ya kiafya, alisema anamshukuru Rais Magufuli kwani kwa sasa hali yake imeimarika baada ya kupata msaada wa matibabu.
“Awali nilikuwa na atembetea kwenye wheel chair  lakini kwa sasa ninaweza alau kusimama kwa msaada wa magongo.  Sina la kusema zaidi ya kusema asante Rais Magufuli nasi Watanzania tunakuombea kwa Mungu akupe afya njema ili uweze kuongoza taifa letu kwa upendo kama unavyofanya sasa,” alisema


 
NA MWANDISHI MAALUM, DODOMA

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Peter Mavunde amewataka wananchi wa Jimbo la hilo kushirikiana na serikali na Viongozi wao katika kujiletea maendeleo na kutoa wito kwa jamii kujitoa kwa dhati kuchangia maendeleo kama wanavyofanya kwenye shughuli mbalimbali za kijamii hasa katika sherehe mbalimbali zikiwemo harusi.

Mhe. Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira ameyasema hayo leo Agosti 25, 2018 wakati akiongoza mamia ya wananchi wa kata ya Kikuyu-kusini katika ujenzi wa vyumba vya madarasa  Jijini Dodoma ambapo Mbunge huyo amechangia matofali 1,000 na mifuko ya Saruji 130, Computer 1, Jezi, mipira pamoja na kusimika magoli ya chuma katika uwanja wa michezo uliopo katika Shule ya Msingi Kikuyu B.
Akimuunga mkono Mhe. Mavunde, Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe. Omary Badwell amewapongeza wananchi wa Kata ya Kikuyu Kusini kwa muitikio wao mkubwa kwenye shughuli za maendeleo na kuahidi kushirikiana na Mhe. Mavunde kutatua changamoto za shule hiyo kwa kuchangia mifuko 20 ya Saruji iliyopo eneo ambalo na yeye ni mkazi wake na watoto wake pia wanasoma katika shule husika. 

Aidha Diwani wa kata ya Kikuyu Kusini Mhe. Kutika amemshukuru Mhe. Mbunge Mavunde kwa kusaidia kutatua kero hiyo ya ukosefu wa vyumba vya madarasa na hivyo ujenzi huo utasaidia kuboresha miundombinu ya shule hiyo na hivyo kuchukua wanafunzi wengi kwa wakati mmoja.

 Mhe. Mbunge akiwa na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kikuyu B.
 Mhe. Mavunde akikabidhi moja kati ya mifuko 130 ya saruji.





No comments :

Post a Comment