Bw.
Addo Komba Afisa kutoka Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo,
akikabidhiwa kombe kufuatia ushindi timu ya mpira wa miguu ya Wanawake
ya Tanzania kwenye Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki lililofanyika
Bujumbura, Burundi.
NA MWANDISHI MAALUM, BUJUMBURA
Tamasha
la Kwanza la Michezo la Jumuiya ya Afrika Mashariki lililokuwa
likifanyika jijini Bujumbura limefikia tamati leo tarehe 29 Septemba,
2018. Hafla ya kufunga tamasha hilo ilihudhuriwa na Viongozi waandamizi
wa Serikali kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Wananchi kutoka maeneo
mbalimbali ya nchini Burundi. Akizungumza katika hafla hiyo
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Liberatus
Mfumukeko alisema maadhimisho ya tamasha hilo yameleta tija kubwa
katika kuleta na kuimarisha umoja na shirikiano, kuibua na kuendeleza
vipaji mbalimbali vya wananchi wa Afrika Mashariki.
Mhe.
Sindimwo Gaston Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi, kwa upande
wake amesema ni fahari kubwa kwa Burundi kuandaa tamasha hilo
lililofanyika kwa kipindi cha wiki mbili. Aliongeza kusema washiriki wa
wamichezo hiyo watakuwa mabalozi wa kuelezea sifa nzuri za amani na
utulivu ulipo nchini Burundi tofauti na inavyosemwa na baadhi ya watu. Katika
tamasha hilo Tanzania imeshinda kombe moja la mpira wa miguu wa
wanawake ,medali ya fedha katika riadha, mpira wa pete na karatee. Tamasha hili lilifanyika kuanzia tarehe 16 hadi 29 Agosti 2018, katika Jiji la Bujumbura na Gitega nchini Burundi. |
No comments :
Post a Comment