Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akitoa
pole kwa shule ya sekondari ya Kimbiji katika maombolezo ya vifo vya
wanafunzi wanne.
Wanafunzi wa sekondari ya Kimbiji wakiwa katika huzuni kubwa ya kifo cha wenzao wanne.
Wanafunzi wa sekondari ya Kimbiji wakiwa katika huzuni kubwa ya kifo cha wenzao wanne.
Watumishi wa
Kigamboni pamoja na wazazi walipoungana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo kwenye
maombolezo ya vifo vya wanafunzi wanne.
SERIKALI imesikitishwa
na vifo vya wanafunzi wanne ambao ni wasichana wa kidato cha nne kutoka
shule ya sekondari Kimbiji iliyopo Kigamboni jijini Dar es salaam
waliofariki kwa ajali ya
maji walipokuwa wakiogelea katika bahari ya
Hindi.
Vifo vya wanafunzi hao
vilitokana na sherehe iliyoratibiwa na shule husika ili kuwapongeza
wanafunzi hao wa kidato cha nne baada ya kufanya vyema mitihani yao ya
kujipima.
Akizungumza kwa majonzi
shuleni hapo,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amesema serikali imepokea kwa
masikitiko vifo hivyo na kutoa pole kwa wanafunzi, wazazi, na walimu wa
shule hiyo kwa msiba huo mzito.
Waziri Jafo amewataka walimu wote nchini kujiepusha na ufanyaji wa sherehe za wanafunzi katika mazingira hatarishi.
Aidha, Waziri Jafo aliwasilisha rambirambi kwa familia nne za wafiwa.
Wanafunzi waliofariki dunia ni Secilia Ernest Paulo, Selestina Vitus Malipesa, Agnetha Philipo Mlaki na Queen Leonard Mandala.
No comments :
Post a Comment