Lucy Ngowi
MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade)
inaanzisha soko lijulikanalo 'Soko la Sabasaba Vunja Bei Bonanza’ kila
Jumamosi na Jumapili kuanzia Julai 28, mwaka huu, lengo likiwa ni
kuwawezesha wananchi kununua bidhaa zenye punguzo la bei.
Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade, Edwin Rutageruka amesema Dar es Salaam
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu soko litakalofanyika
katika viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.
Amesema soko hilo ni ubunifu wao kuwezesha wafanyabiashara wadogo, wa
kati na wakubwa pamoja na wenye viwanda kufanya biashara ili wapate
soko endelevu la bidhaa na wananchi wanufaike na punguzo kupitia bidhaa
hizo.
Alisema pia wanawaalika wafanyabiashara wa nje kushiriki katika soko
hilo, ilimradi wafanyabiashara wote watoe bei maalumu zenye punguzo.
Kwa upande mwingine alisema, kwenye soko hilo kutakuwa na michezo na
burudani mbalimbali ambayo itatoa burudani kwa watoto na watu wazima,
pamoja na nyama choma.
Alisema hadi kufikia jana tayari kampuni 108 za hapa nchini zilikuwa
zimejiandikisha kwa ajili ya kuuza bidhaa zao, lakini bado wanaendelea
kupokea maombi kwa wahitaji.
Meneja wa Mradi huo wa ‘Vunja Bei Bonanza,’ Samsonite Odera amesema,
walitumia miaka miwili kutengeneza mifumo ya mradi huo, kwa kuwa waliona
imefika mahali pa kutengeneza mifumo ya wafanyabiashara kupata nafasi
ya soko la pamoja
No comments :
Post a Comment