WAKATI aliyekuwa Mbunge wa Monduli kupitia
Chadema, Julius Kalanga akitangaza kujiuzulu nyadhifa zake, ikiwemo
kuachia nafasi yake ya ubunge na kujiunga CCM, baadhi ya wasomi na
wanasiasa wamebainisha kuwa uongozi mzuri wa Rais John Magufuli, ndio
chanzo cha viongozi wa
upinzani kuhama vyama vyao.
Mpaka sasa madiwani zaidi ya 40 na wabunge watano, wamehama vyama ikiwemo Chadema na Chama cha Wananchi (CUF) na kujiunga na CCM. Wengi wao wanadai wanavutiwa na utendaji wa Rais Magufuli na kulalamikia sera mbovu katika vyama walivyotoka.
Kalanga alirejea CCM juzi usiku mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole. Alisema kuwa amefanya hivyo kwa hiari yake mwenyewe.
Wakizungumza na gazeti hili wachambuzi wa masuala ya siasa kuhusu kuhama viongozi hao na kujiunga na CCM, walisema vyama vingi vimekosa sera za kuwavutia, jambo ambalo linawafanya kukata tama na kuondoka.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) katika Idara ya Sayansi ya Siasa, Benson Bana alisema viongozi wanaovihama vyama vyao na kujiunga na CCM, wanaangalia chama kilivyojipanga na kuvutiwa na jinsi wanavyofanya kazi.
Amesema wote wanaohama, wanapiga hesabu katika uchaguzi wa mwaka 2020 kuwa vyama vyao vitakuwa katika nafasi gani, hasa ukizingatia utendaji mzuri unaofanywa na Rais Magufuli, ambao umekuwa ukivutia siku hadi siku.
Aliongeza kuwa viongozi wengi wanapojiunga na chama, wanaangalia mambo mengi zikiwemo sera nzuri zinazotekelezeka, lakini wakizikosa wanaweza kukimbia, kwa kuwa kila mwananchi ana haki ya kujiunga na chama chochote.
Bana alisema ni muhimu kwa sasa vyama vya upinzani, vianze kujitathimini na kujijenga upya kama havitaki kuendelea kuiona ‘hamahama’ inayoendelea kwa kasi.
“Lazima wajipime ili waimarishe vyama vyao, lazima vyama viibue sera ili watu wavutiwe kama hawataki kuona hii hamahama inayoendelea, haiwezekani madiwani zaidi ya 40 na wabunge waondoke, ni lazima wajitathimini,” alisema Bana.
Spika mstaafu Pius Msekwa alisema viongozi wanaohama, wanavutiwa na kitu au wanasukumwa na jambo ambalo hawalipati huko wanakotoka.
“Hawa wabunge wa Chadema wapo katika makundi haya mawili ya kuvutiwa pamoja na kusukumwa na jambo ambalo hawalipati huko walipotoka, wengi wakizungumza wakati wanahama utawasikia wakisema haya,” alisema.
Alisema viongozi hao wamevutiwa na utendaji wa Rais Magufuli, ambao umewafanya kutaka kuja ili kumuunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yake.
Mwenyekiti wa CCM mkoani Arusha, Lootha Sanare, akimzungumzia Kalanga, amesema amempomkea kwa mikono miwili na kuwataka viongozi wengine wa upinzani kuacha kusuasua na kujiunga na CCM.
Sanare amesema, muziki wa CCM kwa sasa ni mzito na wenye kishindo hasa mkoani Arusha.
Alieleza kuwa kwa wale wanaoendelea kubaki Chadema ambako hakuna demokrasia, wahame haraka kwani CCM itajaribu mitambo yake katika uchaguzi wa mwakani wa serikali za mitaa na watashinda kwa kishindo.
Amesema CCM Arusha inaandaa mikakati madhubuti ya kuhakikisha majimbo yote yaliyochukuliwa na Chadema, kwanza yanarudi CCM na halmashauri zilizo chini ya chama hicho cha upinzani, pia zinarejeshwa CCM, kwa sababu ya sera zuri za chama hicho kinachoongozwa na Rais Magufuli.
Mwenyekiti huyo amesema wabunge, madiwani na wafuasi wa Chadema, wanarudi CCM baada ya kuona sasa sera zote zilizokuwa zikitamkwa na kupigiwa kelele na wapinzani, zinafanywa na chama tawala kwa kishindo chini ya Rais Magufuli.
Alisema kasi anayoenda nayo Rais Magufuli ni ya kimbunga, ambayo inaonesha wazi mpaka mwakani katika uchaguzi wa serikali za mitaa, wananchi wengi wataichagua CCM na huo ndio utakuwa mwisho wa upinzani nchini.
''Uongozi bora wa Rais Magufuli ndio unawapa kiwewe wabunge na madiwani wa upinzani na kuona sasa hawana jipya na kuamua kujiunga na CCM.''
Mkongwe wa CCM Jijini Arusha, Modest Meikoki yeye amesema kasi ya Rais ya kupambana na ufisadi, ubadhirifu wa mali za umma na kuwaweka ndani watendaji wa serikali na taasisi za umma waliofanya ubadhirifu miaka ya nyuma ni hatua iliyokuwa ikisubiriwa kwa asilimia kubwa na wananchi wa nchi hii.
Meikoki alisema hoja hizo, ndio zilikuwa ngao ya upinzani katika majukwaa, lakini kwa sasa hawana namna ya kufanya ni kuamua kujiunga na chama hicho tawala tu na sio vinginevyo, kwani hawana jipya tena majukwaani.
Alisema wabunge na madiwani wa upinzania, kila kukicha wanarudi CCM na kusema wanaunga mkono jitihada za Rais Magufuli.
“Sasa wewe uliobaki huko upinzani utakuwa na hoja gani katika uchaguzi wa mwakani wa serikali za mitaa, kilichobaki ni kurudi chama tawala,” alisema.
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Elias Mpanda alisema kuwa milango iko wazi kwa wale wote waliokengeuka katika uchaguzi mkuu uliopita kwa kufuata mkumbo.
Alisema kuwa chama tawala, kina demokrasia iliyotukuka katika kupeana nafasi za uongozi na sio kukumbatia uongozi kama wa kifalme.
Mpanda aliwataka wabunge na madiwani ambao bado wako upinzani, kufanya hivyo mapema iwezekanavyo kwani huko waliko hakuna usawa wala demokrasia kwani wanaongea midomoni, lakini vitendo hakuna.

No comments :
Post a Comment