SERIKALI imetangaza leo kuanza rasmi kwa Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), huku ikiwatoa hofu
wanachama wa mifuko inayoungwanishwa na kuwataka wakurugenzi kutoa mafao
kwa wakati na kuzingatia sheria.
Aidha, wajumbe wanane kati ya tisa wanaounda Bodi ya Mfuko wa PSSSF wametangazwa rasmi. Hatua ya kuanza kutumika Sheria ya PSSSF Namba 2 ya mwaka 2018, imetangazwa jana mjini hapa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama alipozungumza na waandishi wa habari.
"Napenda kuchukua fursa hii kuwajulisha kuwa serikali imekamilisha maandalizi yote muhimu ya utekelezaji wa sheria ya PSSSF na imeridhia kwamba mfuko huo unaweza kuanza rasmi kutekeleza majukumu yake. Aliongeza:
"Nikiwa Waziri mwenye dhamana ya Hifadhi ya Jamii na kwa mamlaka niliyonayo chini ya Kifungu cha 1(1) cha Sheria ya PSSSF nimeteua Agosti mosi mwaka 2018 kuwa ndiyo tarehe rasmi ya kuanza kutumika kwa Sheria ya PSSSF."
Sheria hiyo inaunganisha mifuko minne ya PSPF, LAPF, PPF na GEPF na kuunda mfuko mmoja wa PSSSF kwa ajili ya watumishi wa umma. Muswada huo ulipitishwa na Bunge Januari 31, mwaka huu na kusainiwa na Rais John Magufuli Februari mwaka huu, hivyo kuwa sehemu ya sheria za nchi.
Mhagama alisema watumishi wote waliokuwa katika mifuko inayounganishwa, watahamishiwa katika mfuko mpya na watapangiwa majukumu kwa kuzingatia muundo wa mfuko huo.
Alisema rasilimali, vitega uchumi, mikataba na madeni yote ya mifuko hiyo pamoja na stahiki zote za wanachama wa mifuko inayounganishwa, wakiwemo wastaafu na warithi wao, zitahamishiwa katika mfuko mpya na wanachama wataendelea kupata huduma kama kawaida.
"Nawaagiza Wakurugenzi (Eliud Sanga –PSSSF na William Erio-NSSF), kuhakikisha wanakusanya michango ya wanachama na kuwaingiza wanachama wapya, pia wahakikishe mafao kwa wanaufaika yanalipwa kwa wakati na kwa viwango vilivyowekwa na sheria.
"Pia wahakikishe wanasimamia ipasavyo vitega uchumi vyote ili kuhakikisha vinaleta faida ambayo itasaidia kuwalipa wanachama mafao yao."
Aidha, Mhagama aliwatoa hofu wanachama wa mifuko iliyounganishwa, wadau wa sekta hiyo na wananchi kwamba serikali imelifanyia kazi, jambo hilo kwa umakini mkubwa ili kusiwe na athari zozote.
"Serikali imehakikisha michango, mafao, rasilimali, vitega uchumi, uwekezaji na miradi mbalimbali ya mifuko iliyounganishwa inaendelea kuwa salama kwa maslahi ya wanachama na nchi," alisema.
Alisema serikali kwa kupitia Mamlaka ya Usimamizi ya Mifuko, imeandaa mkakati maalumu wa kutoa elimu kwa umma kuhusu Sheria na Kanuni za PSSSF ili kuhakikisha kwamba wanachama na wadau wote wa sekta wanakuwa na uelewa sahihi wa sheria hizi na mabadiliko yaliyofanyika.
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Eliud Sanga alisema atahakikisha anafanya kazi kwa weledi wa juu ili kuweza kuondoa changamoto na kero ili kuwanufaisha wanachama.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio alisema kuwa mifuko umejipanga kutoa huduma bora zaidi kwa wanachama, ikiwa ni pamoja na kutoa mafao yao kwa wakati kwa mujibu wa sheria mpya.
Katika hatua nyingine, Jenista amewateua wajumbe wa Bodi ya PSSSF ambao ni Leah Ulaya na Rashidi Mtima, ambao ni Wawakilishi wa Wafanyakazi kutoka Chama cha Wafanyakazi chenye Wanachama wengi kwenye mfuko wa PSSSF.
Wengine ni Dk Aggrey Mlimuka na Stella Katende ambao ni wawakilishi wa waajiri kutoka Chama cha Waajiri, chenye uwakilishi mkubwa pia kuwa wajumbe katika mfuko huo.
Wajumbe wengine ni Thomas Manjati kutoka sekta binafsi, Henry Katabwa kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suzan Kabogo kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Jacob Mwinula kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.
"Nafasi ya mjumbe mmoja kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itatangazwa muda si mrefu baada ya taratibu husika kukamilika," alisema Jenista.

No comments :
Post a Comment