Rais
wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wanakijiji wa
Rubambagwe plot (Chato) wakati alipokwenda kutoa pole kwenye msiba wa
Patricia
Tibengana Mazigo 75 aliyefariki juzi tarehe 16-8-2018 Chato mkoani
Geita. Wakati
huo huo Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw Gerson Msigwa,
ameandika kwenye ukurasa wake wa Tweeter kuwa Rais Magufuli amefiwa na
dada yake, Bi.Monica Joseph Magufuli,
aliyekuwa amelazwa kwenye wodi ya uangalizi maalum (ICU), ya hospitali
ya
Bugando jijini Mwanza. Bi. Mo nica
amefariki ikiwa ni siku moja tu baada ya Rais kufika hospitalini hapo kumjulia
hali. (PICHA NA IKULU)
Katika picha hii ya maktaba iliyopigwa na Ikulu inamuonyesha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akimjulia hali Dada yake Monica Joseph Magufuli ambaye amelazwa katika
Chumba cha uangalizi Maalum ICU katika hospitali ya Bugando mkoani Mwanza leo Agosti 18, 2018.
Marehemu Monica Joseph Magufuli, Enzi za uhai wake
Marehemu Monica Joseph Magufuli, Enzi za uhai wake
No comments :
Post a Comment