Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) akioneshwa ramani inayoonesha Ziwa Ngozi
ambalo ni miongoni mwa vivutio vya utalii katika Pori la Akiba la Kimisi na
aliyekuwa Meneja wa Pori hilo Bigilamungu Kagoma wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana pori hilo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua
ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika
pori hilo lililopandishwa hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa.
NA LUSUNGU HELELA-KAGERA
BAADA ya kuyapandisha hadhi mapori matano ya akiba, Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amewataka wawekezaji wa ndani
na nje ya nchi wachangamkie fursa ya kuwekeza katika Mapori hayo.
Aidha, Amesema Serikali imefuta kodi ya kuingiza magari ya
watalii nchini ili kuwawezesha wananchi walio wengi kuingia katika
biashara hiyo ikiwa lengo ni kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya
Utalii.
Ametaja aina ya uwekezaji unaohitajika kuwa ni ujenzi wa hoteli
zenye hadhi ya nyota moja hadi zenye nyota tano, nyumba za kulala wageni,
uanzishwaji wa makampuni ya utalii pamoja na kutoa huduma za vyakula kwa ajili
ya watalii.
Ametoa rai hiyo leo wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na
Usalama wilayani Karagwe mkoani Kagera kabla ya kutembelea ziwa Ngoma
ambalo ni miongoni mwa vivutio vya utalii vilivyopo katika Pori la Akiba la
Kimisi ambalo ni miongoni mwa mapori yaliyo katika mchakato wa kuwa hifadhi za
taifa.
Naibu waziri huyo anatembelea mapori ya mkoa wa Kagera
kufuatilia hatua iliyofikiwa na Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA)katika
kuyaendeleza.
Amesema Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na
Rumanyika ni hazina na fursa kwa mikoa ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania
kufunguka kiutalii kwa wananchi wa maeneo hayo na taifa kwa ujumla.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( katikati) akisalimiana na baadhi ya
wafanyakazi wakati alipowasili katika ofisi za wilaya ya Karagwe kabla ya
kutembelea jana pori la akiba Kimisi katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua
ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika pori hilo lililopandishwa
hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa,
Wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Karagwe, Godfrey Luheluka
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Japhet Hasunga akisaini kitabu cha
wageni mara alipowasili katika ofisi za
wilaya ya Karagwe kabla ya kutembelea jana pori la akiba Kimisi katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua
ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA
katika pori hilo lililopandishwa hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi
za Taifa.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja
na baadhi ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ngala pamoja na baadhji
ya watumishi wa TAWA na TANAPA wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana pori hilo katika ziara
yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa
ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika hilo. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU
HELELA-WMU)



No comments :
Post a Comment