Sunday, August 26, 2018

MKUTANO WA 7 WA UMOJA WA MACHIFU TANZANIA WAANZA HUKO ROMBO KILIMANJARO


  Chifu Emmanuel Zulu Gama kutoka kabila la Wangoni Mkoani Ruvuma, akimwomba  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe(hayupo pichani) ofisi yake kushiriki katika Tamasha la Mashujaa waliyopigana Vita ya Majimaji linalofanyika kila Mwaka Mwezi Februari mkoani Ruvuma, katika ufunguzi Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe(katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa machifu ulioanza Agosti 26, 2018 huko Marangu, mkoani Kilimanjaro.Pamona na mambo mengine, Dkt. Mwakyembe amewaagiza Maafisa Utamaduni Mkoa na Wilaya nchini kukamilisha ukusanyaji wa maoni ya wadau wa Sekta ya Utamaduni kwa ajili ya kuboresha Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997. Kushoto ni Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi.Lilian Beleko kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania Chifu Frank Marrialle (kushoto) akitoa ahadi ya umoja huo kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya kuboresha Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997 kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe(hayupo pichani) katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro,kulia kwake ni Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia) akikabidhi nakala 21 za Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997 kwa Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela (kushoto) katika Ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania,uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kugawa kwa Machifu waliyoshiriki Mkutano huo ili waweze kutoa maoni yao kutokana na mapungufu ya sera hiyo inayofanyiwa marekebisho.

 Chifu Nshoma Hawa wa Ukamba Kahama akieleza  changamoto zinazomkumba katika ikulu yake ambapo ardhi ya himaya yake iliyozikiwa machifu wenzake kuporwa na kugawiwa kwa wananchi kwa ajili ya kilimo kinyume na utaratibu wa uhifadhi wa ardhi za makazi ya machifu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) katika Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe aliyeketi (watano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja  na baadhi ya Machifu wa Tanzania mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa  Umoja wa Machifu Tanzania uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro,wanne kulia ni Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela,na wanne kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania Chifu Frank Marrialle.

No comments :

Post a Comment