Balozi wa Kuwait nchini Tanzania,
Jasem Al-Najem akizungumza na wazazi wa watoto ambao wanatibiwa saratani
katika hospitali hiyo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Suleiman Saleh na Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Red Crescent
kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania,
Jasem Al-Najem akizungumza na Ofisa Mtendaji wa Tumaini la Maisha (TLM),
Dkt. Trish Scanlan baada ya ofisa huyo kumweleza mahitaji wanahitaji
watoto wanaotibiwa saratani katika hospitali hiyo. Kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suleiman Saleh, kulia ni Naibu
Mwenyekiti wa Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi (mwenye koti)
na wengine ni wawakilishi wa Jumuiya ya Red Crescent.
Balozi huyo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto baada ya kupewa zawadi mbalimbali.
Balozi
wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem ametembelea Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) na kuahidi kuwasaidia watoto wenye saratani ambao
wanatibiwa katika hospitali hiyo.
Katika
ziara hiyo balozi huyo alimtaka Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tumaini la
Maisha (TLM) katika hospitali hiyo, Dkt. Trish Scanlan kumwandikia
mahitaji ambayo watoto hao wanapaswa kupatiwa ili aweze kushiriki katika
kuwapatia tiba pamoja na mambo mengine.
Balozi
huyo aliongozana na Naibu Mwenyekiti wa Red Crescent kutoka Kuwait,
Anwar Alhasawi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati-Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Suleiman Salehe
pamoja na pamoja na viongozi mbalimbali wa Lions Club ambayo imekuwa
ikiwasadia watoto hao mahitaji mbalimbali.
Pia,
balozi huyo alitembelea watoto wenye saratani katika jengo la watoto
pamoja na kuwapatia zawaidi mbalimbali ikiwamo vifaa vya kuchezea.
Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa mwezi
imekuwa ikipokea wastani wa watoto 30 hadi 40 wenye saratani ya aina
mbalimbali. Wengi wa watoto wanaopokelewa wamekuwa wakisumbuliwa na
saratani ya damu, jicho, figo na saratani ya matezi.
No comments :
Post a Comment