Friday, July 20, 2018

WAZIRI MHAGAMA AMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA KUUNGANISHA DARAJA LA NYERERE, KIGAMBONI


Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimueleza jambo Mhandisi Jamal Mruma, anayejenga kwa kiwango cha lami barabara yenye urefu wa  kilometa mbili inayo unganisha Daraja la Nyerere na barabara ya Kibada -Feri iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati akikagua ujenzi wa barabara hiyo. Wakwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio.
 Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza  Mhandisi Jamal Mruma, anayejenga kwa kiwango cha lami barabara yenye urefu wa  kilometa mbili inayo unganisha Daraja la Nyerere na barabara ya Kibada -Feri iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati akikagua ujenzi wa hiyo. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NMSSF, Bw. William Erio.

Mmoja wa Wananchi akikamilisha taratibu za malipo katika Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Daraja la kigamboni tangu lianze kufanya kazi  mwezi Mei mwaka 2016 hadi Juni 2018,  takribani shilingi bilioni 17.1 zimekusanywa na  kwa wastani kila mwezi mapato ya shilingi milioni 600 hukusanywa.

No comments :

Post a Comment