Friday, July 20, 2018

MARAFIKI WA KWELI: LOWASSA AMFARIJI JK KWA KUFIWA NA BABA MKWE WAKE, WAKUTANA MSIBANI DAR


Rais mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, (kushoto), akisalimiana na Waziri Mkuu (mstaafu) ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Mhe. Edward Lowassa, wakati akimpokea nyumbani kwake Msasani kwenye msiba wa baba mkwe wake leo Ijumaa Julai 20, 2018. Wawili hao wanao urafiki wa muda mrefu ambao mara kadhaa wamewahi kuutangaza hadharani.
Mama Salma Rashid Kikwete Mke wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amefiwa na Baba yake Mzazi Mzee Rashid Mkwachu. Na mazishi yalitarajiwa kufanyika Alasiri hii kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

No comments :

Post a Comment