Tuesday, July 17, 2018

TUTAPELEKA MILIONI 300 KUPANUA JENGO LA WAZAZI HOSPITALI YA KITETE TABORA: WAZIRI UMMY

  WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iemahidi kupeleka shilingiu milioni 300 kupanua jingo lka wazazi Hospitali ya Rufaa Kitete mkoani Tabora.

Hayo yemesemwa leo Julai 17, 2018 na Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Ummy Mwalimu, (pichani) katika ukurasa wake wa Facebook, ambapo alifanya ziara kwenye hospitali hiyo kufuatilia utoaji wa huduma za afya na kubaini moja ya changamoto kubwa inayoikabili hospitali hiyo ni udogo wa jingo la wazazi.

“ Leo nipo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Kitete kufuatilia utoaji wa huduma za Afya. Changamoto kubwa ni uhaba wa watumishi hasa wauguzi na ufinyu wa Wodi ya Wazazi. Mwezi huu tumepeleka Wauguzi wapya 39 na watumishi wengine 10. Aidha, tunaleta shs 300m kupanua jengo la Wazazi na kukamilisha Chumba cha Upasuaji (Theatre)” Alisema Mhe. Waziri.



No comments :

Post a Comment