Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa
Mlipakodi Bw. Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
akizungumzia juu ya TRA ilivyojipanga katika kutoa huduma kwa wananchi
katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yaliyoanza
tarehe 28 Julai, 2018 jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi
ambaye pia ni Mratibu wa Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama
Sabasaba kwa upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Honester
Ndunguru (kushoto) akijadiliana jambo na Maafisa wa Kodi wakati wa
maonyesho hayo yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba
jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bi. Mercy Macha akitoa elimu ya kodi kwa wananchi
waliotembelea Banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu
kama Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es
Salaam.
Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bi. Judith Lwaikondo akimhudumia mwanachi aliyetembelea
Banda la TRA kwa ajili ya kupata huduma wakati wa Maonyesho ya 42 ya
Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya
Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja wakitoka katika
Banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa Maonyesho ya 42 ya
Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya
Sabasaba jijini Dar es Salaam. Banda la TRA lipo mkabala na banda la
Azam ndani viwanja vya Sabasaba.
PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO
…………………
Na Veronica Kazimoto
Dar es Salaam
1 Julai, 2018
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea kutoa huduma mbalimbali ikiwa ni
pamoja na kupokea maoni na mrejesho kutoka kwa wananchi, usajili wa
walipakodi na kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa manufaa ya
wananchi wote kwa ujumla.
Akizungumzia
juu ya TRA ilivyojipanga katika kutoa huduma kwa wananchi katika
Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba, Mkurugenzi wa Huduma
na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo amesema kuwa, wananchi
watumie fursa hii kujifunza masuala mbalimbali ya kodi ili kuongeza
uelewa na uhiari wa ulipaji kodi.
“Sisi
kama Mamlaka tumejipanga kuhakikisha kuwa, tunatoa huduma kwa kila
mwananchi atakayetembelea banda letu na tunapokea maoni na mrejesho
kutoka kwa wananchi. Vilevile tunasajili walipakodi, tunawaelimisha
wananchi umuhimu wa kulipa kodi, tunaelezea haki na wajibu wa Mlipakodi
kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Huduma na Mlipakodi pamoja na
kuwaonyesha makusanyo yote ya miaka mitatu ya fedha iliyopita yaani
kuanzia 2015/16, 2016/17 na 2017/18,” alisema Kayombo.
Kayombo
ameongeza kuwa, makusanyo yanayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania
ndiyo hutumika katika kutoa huduma mbalimbali za jamii ikiwemo
miundombinu ya barabara na umeme, maji safi na salama, elimu pamoja na
huduma za afya.
Naye
Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi ambaye pia ni Mratibu wa maonyesho hayo
kwa upande wa TRA Bi. Honester Ndunguru ametoa wito kwa wananchi
kujitokeza kwa wingi katika banda la TRA ili waweze kupata elimu sahihi
ya kodi na hatimaye waweze kulipa kodi stahiki na kwa wakati.
“Kila
mwaka tunashiriki maonyesho haya ya Sabasaba lakini kwa mwaka huu
tumejipanga vizuri zaidi hivyo nachukua fursa hii kuwaomba wananchi
kujitokeza kwa wingi katika banda letu ili tuwahudumie na kuwaelimisha
juu ya masuala mbalimbali ya kodi na hatimaye waweze kulipa kodi sahihi
na kwa wakati unaotakiwa,” alisema Ndunguru.
Banda
la Mamlaka ya Mapato Tanzania linapatikana ndani ya viwanja vya
Sabasaba na lipo mkabala na banda la Azam ambapo wananchi wanaendelea
kupata huduma mbalimbali zinazotolewa ndani ya banda hilo.
No comments :
Post a Comment