Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akimkabidhi
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza (wa kwanza kulia) ramani ya
maeneo yanayopata mawasiliano mkoani humo wakati wa ziara ya Kamati ya
Bunge ya Miundombinu ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa
huo. Anayeshuhudia katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.
Hawa Mchafu
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akiteremka
kwenye kilima kilichojengwa mnara wa mawasiliano wakati wa ziara ya
Kamati ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano
kwenye kijiji cha Mkulula kilichopo Kata ya Malenga Makali mkoani
Iringa. Wa pili kulia ni mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Bhagwanji Meisuria
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu akifafanua jambo kwa wajumbe wa
Kamati hiyo na watendaji (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza (wa kwanza kushoto)
wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano
kwenye mkoa huo. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akisaini kitabu cha wageni
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa wananchi wa
kijiji cha Mkulula kilichopo Kata ya Malenga Makali mkoani Iringa wakati
wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua upatikanaji wa
mawasiliano kwenye mkoa huo. Wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa
Kamati hiyo Mhe. Hawa Mchafu na wa kwanza kulia ni mjumbe wa Kamati hiyo
Mhandisi Ramo Makani
Mwenyekiti wa kijiji cha Mkulula
kilichopo Kata ya Malenga Makali mkoani Iringa Bwana Samwel Mbande
akiishukuru Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa kufika kijijini hapo
wakati wa ziara yao ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa
huo. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Atashasta Nditiye na wa tatu kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati
hiyo Mhe. Hawa Mchafu
Wanakiji wa kijiji cha Mkulula
kilichopo Kata ya Malenga Makali mkoani Iringa wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo
pichani) kuhusu jitihada za Serikali za kuwapatia wananchi mawasiliano
wakati wa ziara ya
Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwenye kijiji hicho ya
ukagua upatikanaji wa mawasiliano.
………………………………………………………………………..
Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania imeyataka makampuni ya simu nchini kutoa huduma za data kwa
wananchi waishio vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara ambapo
makampuni hayo yamejenga minara kwa ajlii ya kuwapatia wananchi
mawasiliano
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri
wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Ndiye wakati wa ziara ya
Kamati ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua upatikanaji wa huduma za
mawasiliano kwa wananchi waishio viijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa
kibiashara wakati akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Mkulula
kilichopo Kata ya Malenga Makali mkoani Iringa
Nditiye amefafanua kuwa kampuni
za simu zinatoa huduma ya sauti tu yaani 2G kwenye minara ya mawasiliano
waliyojenga badala ya kutoa huduma ya data kwenye maeneo hayo ili
wananchi wapate huduma ya intaneti. Amesema kuwa Serikali kupitia Mfuko
wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inatoa ruzuku kwa makampuni hizo ili
wajenge minara. “Tunataka wananchi wapate mawasiliano kwa kuwa wanalipia
na ni haki yao ya msingi kuwasiliana na hii ndio Serikali ya Dkt. John
Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhudumia
wananchi wa hali zote,” amesema Nditiye.
Ameongeza kuwa hadi sasa UCSAF
imetoa ruzuku kwa makampuni ya simu ambapo jumla ya kata 530 zimepatiwa
huduma ya mawasiliano kwenye maeneo mbali mbali nchini na ujenzi wa
mnara mmoja una gharimu kati ya kiasi cha shilingi milioni mia mbili
hadi milioni mia tatu.
Akiwa katika ziara hiyo, Makamu
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Hawa Mchafu amesema kuwa makampuni ya
simu yanapowekeza yasiwekeze kwa mahitaji ya kipindi kifupi bali
miundombinu ya mawasiliano wanayojenga izingatie mahitaji ya muda mrefu
kwa kuwa wananchi wanaongezeka kwenye maeneo hayo na wanakuwa wengi
mathalani kwenye eneo la kata hiyo wananchi wananchi wanafanya shughuli
za uchimbaji wa madini, kilimo na ufugaji wa samaki.
Ameongeza kuwa watoa huduma
waweke mawasiliano ya data yaani 4G ili wananchi wapate huduma.
“Haiwezekani fedha imetolewa na Serikali ya kujenga mnara kiasi cha
shilingi milioni 260 halafu wananchi hawawasiliani,” Mhe. Mchafu
amesema. Amefafanua kwa wanakijiji hao kwa kusema kuwa, “mnara mnauona
umejengwa na TIGO kwa kupatiwa ruzuku na Serikali kupitia UCSAF kiasi
cha shilingi milioni 260, nawaomba muiamini Serikali kuwa itatua kero
zenu” Mhe. Mchafu amesema.
Naye mwanakijiji wa kijiji hicho
Bwana Patrick Sanga amesema kuwa mawasiliano kwenye maeneo hayo ni
hafifu ambapo wanaiomba Serikali kuhakikisha kuwa mawasiliano hayo
yanaongezwa nguvu ili kuwawezesha wananchi kuwasiliana vizuri muda wote.
Meneja Msaidizi wa Kitengo cha
Ufundi wa kampuni ya TIGO-Iringa Bwana Geofrey Anitike Mwaitenga amesema
kuwa wamepokea maelekezo na wataongeza nguvu ya mawasiliano hayo kwa
kuwa watu wameongezeka na kumekuwa na mahitaji makubwa ya mawasiliano
kutokana na uwepo wa shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahab katika
kijiji cha Nyakavangala kilichopo kwenye kata hiyo na ufugaji wa samaki
kwenye maeneo hayo tofauti na hapo awali kabla mnara haujajengwa.
Naye Mkuu wa Uendeshaji wa UCSAF
Mhandisi Albert Richard amesema kuwa mnara huo unatoa huduma kwa watu
7,917 wanaoishi kwenye vijiji sita vya Nyakavangala, Isaka, Usolanga,
Makachupa, Mkulula na Mkulula vilivyopo kwenye Kata hiyo.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Iringa Bwana Fikira Kissimba wakati akiwasilisha hali ya mawasiliano
mkoani humo kwa niaba ya Mhe. Masenza mbele ya Kamati hiyo amesema kuwa
UCSAF imefikisha mawasiliano kwenye kata 14 mkoani humo ambapo
mawasiliano hayo yamewawezesha wananchi kupata huduma mbali mbali za
kijamii na uzalishaji mali.
Kissimba amesema kuwa mawasiliano
hayo yamefikishwa kwenye kata hizo na UCSAF kwa kuzipatia ruzuku
kampuni tatu za simu ikiwemo Shirika la Mawasiliano Tanzania ambapo
wamefikisha mawasiliano kwenye kata sita ambazo ni Idodi, Lumuli,
Mahuninga, na Wasa; Vodacom kwenye kata sita ambazo ni Kihorogota,
Nduli, Nyang’oro, Udekwa, Ikweha na Mapanda ambapo TIGO imefikisha
kwenye kata mbili ambazo ni Malenga Makali na Ukwega.
Pia, Kamati hiyo imekagua
upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha mMayala kilichopo kwenye
Kata ya Wanging’ombe mkoani Njombe ambapo UCSAF imetoa ruzuku kwa
kampuni ya Vodacom shilingi milioni 60 ambapo imeshirikiana na Serikali
kujenga mnara huo ambao unatoa huduma za mawasiliano kwenye vijijini
kumi na mbili. Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Bathiweli Mathayo Mlawa
ameileza Kamati kuwa kabal ya kujengwa kwa mnara huo mawasiliano
yalikuwa yanasumbua ila sasa hayasumbui ambapo ameishukuru Serikali kwa
kuhakikisha kuwa wanapata mawasiliano
No comments :
Post a Comment