Naibu Waziri wa uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kushoto) akimkabidhi
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe S. Kebwe (wa pili kulia) picha ya
maeneo yaliyojengwa minara ya mawasiliano na Mfuko wa Mawasiliano kwa
Wote (UCSAF) mkoani humo. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa
Mawasiliano Mhandisi Anjelina Madete na wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu
wa UCSAF Mhandisi Peter Ulanga
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
(aliyesimama) Dkt. Kebwe S. Kebwe akiongea na wajumbe wa Kamati ya Bunge
ya Miundombinu wakati wa ziara yao ya kukagua hali ya mawasiliano
mkoani humo. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na wa pili kushoto ni Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Mhe. Moshi Selemani Kakoso
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Miundombinu (aliyesimama katikati) akiuliza jambo kuhusu hali ya
mawasiliano katika kijiji cha Kaole kilichopo wilayani Mvomero mkoani
Morogoro wakiwa kwenye mnara wa Halotel wakati wa ziara yao ya kukagua
hali ya mawasiliano mkoani humo. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na wan nne kushoto ni
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Peter Ulanga
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa ili kushoto) akifafanua jambo
kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakati wa ziara yao ya
kukagua hali ya mawasiliano katika kijiji cha Kaole kilichopo wilayani
Mvomero mkoani Morogoro. Wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo
Mhe. Moshi Selemai Kakoso na wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi wa
Halotel, Morogoro
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Peter Ulanga akitoa taarifa ya upatikanaji
wa mawasiliano mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakati wa ziara
yao mkoani Morogoro. Waliokaa mbele wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, katikati ni
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moshi Selemani Kakoso na anayefuata ni
Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Kebwe S. Kebwe
Mwenyekiti wa kitongoji cha
Mchanga wa pwani Kaole kilichopo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro,
Bwana Henry Daudi akiishukuru Serikali kwa kufikisha mawasiliano kwenye
kijiji hicho wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu ya
kukagua upatikanaji wa mawasiliano mkoani humo. Wa kwanza kulia ni Naibu
Mkurugenzi wa Halotel, Morogoro Bi……….Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa
Kamati hiyo Mhe. Moshi Selemani Kakoso na wa tatu kulia ni Mtendaji Mkuu
wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Peter Ulanga
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiwa ndani ya gari lake
akiongoza msafara wa wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu ya
kukagua upatikanaji wa mawasiliano katika kijiji cha Kaole kilichopo
wilayani Mvomero mkoaani Morogoro
……………..
Ongezeko la upatikanaji wa huduma
za mawasiliano yamechangia na kuwezesha ukusanyaji wa mapato ya Serikali
katika maeneo mbali mbali nchini.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Dkt. Kebwe Stevene Kebwe mbele ya
Kamati ya Bunge ya
Miundombinu walipotembelea ofisini kwake wakati wa ziara yao ya kukagua
hali ya mawasiliano mkoani humo. Dkt. Kebwe amesema kuwa kadri
mawasiliano yanavyoongezeka yanawezesha ukusanyaji wa mapato mkoani humo
ambapo hadi hivi sasa mkoa huo ni wa pili ukifuatiwa na mkoa wa Dar es
Salaam.
Ameongeza kuwa anayaomba makampuni
mengine ya simu kujitokeza na kujenga miundombinu ya mawasiliano ili
kuongeza upatikanaji wa mawasiliano katika mkoa huo kwa kuwa kiasi cha
asilimia 70 ya eneo la mkoa huo linapakana/linazungukwa na mbuga ya
wanyama ya Selous. Pia, amefafanua kuwa mkoa wa Morogoro ni wa pili kwa
ukubwa ukifuatiwa na mkoa wa Morogoro.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
ya Miundombinu Mhe. Moshi Selemani Kakoso amemueleza Dkt. Kebwe kuwa
maeneo aliyonayo ya kiutawala katika mkoa huo ni makubwa. Kakoso
amesema kuwa kupitia Kamati anayoiongoza wataishauri Serikali ili
kuhakikisha kuwa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inaongeza
upatikanaji wa mawasiliano kwenye maeneo muhimu wanayoona muhimu ya
kiuchumi au ya kiusalama. Aidha, ametoa rai kwa wananchi wanaohujumu
miundombinu ya mawasiliano kwa kuiba betri na sola kwenye minara ya
mawasiliano waache mara moja na ameiomba Serikali ya mkoa huo kudhibiti
jambo hilo.
Wakiwa kwenye kijiji cha Kaole
kilichopo wilayani Mvomero mkoai Morogoro, Mhe. Kakoso ameipongeza
Serikali kwa jitihada walizonazo kupitia UCSAF ya kufikisha mawasiliano
sehemu mbali mbali nchini ambapo hakuna mvuto wa kibiashara ambapo
wananchi wapatao 6,000 wanapata huduma za mawasiliano kwenye kijiji
hicho. Pia, Ameongeza kuwa Kamati imebaini uwepo wa changamoto ya ulinzi
kwenye miradi ya miundombinu ya mawasiliano, usafi na ukosefu wa
mazingira rafiki kwenye maeneo hayo ambapo wakati wa kiangazi moto
unaweza kutokea na kuharibu miundombinu hiyo.
Mhe. Kakoso ameiomba Serikali
kupitia UCSAF kuhakikisha kuwa kunakuwa na mazingira rafiki ya ulinzi na
usalama na usafi kwenye maeneo iliyojengwa miundombinu hiyo ikiwa ni
pamoja na Serikali ya kijiji na wananchi kushirikiana kuilinda
miundombinu hiyo. Amesema kuwa Serikali iweke utaratibu na mwongozo wa
wa kuziwezesha Serikali za vijiji kupara mrabaha na kodi ili kunufaika
na uwepo wa miundombinu ya mawasiliano kwenye maeneo yao.
Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amesema kuwa wako pamoja na
Kamati kwenye ziara ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye maeneo
mbali mbali nchini ambapo tumeshuhudia Serikali ikitoa pesa nyingi za
ili kujenga minara ya mawasiliano ili wananchi waweze kuwasiliana. Pia,
amewaomba wananchi kuendelea kuilinda miundombinu ya mawasiliano iliyopo
kwenye maeneo yao kwa kuwa imejengwa kwa manufaa yao.
Mhandisi Nditiye ameilekeza UCSAF
kuhakikisha kuwa minara iliyojengwa na kampuni ya simu ya Halotel ambayo
haina miundombinu rafiki kwa walinzi ili waweze kukaa dani na kupata
huduma ya choo waweze kujenga miundombinu hiyo ndani ya miwili nchi
nzima.
Mtendaji Mkuuu wa UCSAF Mhandisi
Peter Ulanga akifafanua suuala la changamoto za mazingira rafiki kwenye
miundombinu ya mawasiliano amesema kuwa wanaishukuru Kamati kwa kufika
kwenye maeneo hayo ili Serikali iendelee kuwawezesha na kuendelea
kuboresha mazingira rafiki kwenye miundombinu hiyo.
Ameongeza kuwa hali halisi ya
mawasiliano katika mkoa wa Morogoro ilikuwa ni kwa kiasi cha robo tu ya
eneo la mkoa huo ambalo lilikuwa na huduma za mawasiliano ambapo hadi
sasa katika kipindi cha miaka mitatu, UCSAF imefikisha mawasiliano
katika kata 30 na wataendelea kuweka mawasiliano ili kupunguza kadhia ya
mawasiliano katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Morogoro.
Amefafanua kuwa malengo ya UCSAF
ni kufikisha mawasiliano kwenye kata 45 ambapo kuna changamoto kwa watoa
huduma kujitokeza na kutekeleza miradi hiyo hivyo wataendelea kujifunza
changamoto hizo na kuboresha zaidi.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha
Kaole kilichopo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Bwana Christopher
Henry Daudi ameishukuru Serikali kwa kujenga minara a kufikisha huduma
za mawasiliano. Amesema kuwa mnara wa Halotel uliopo kwenye kijiji hicho
unatoa huduma za mawasiliano kwenye vijiji sita ambavyo ni Kaole
yenyewe, Dihinda, Mziha, Khanga, Bwage na Disinga.
No comments :
Post a Comment