Regina Mpogolo
DAKTARI bingwa wa magonjwa ya damu katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam, Stella Rwezaura
amesema uelewa mdogo katika jamii unasababisha idadi kubwa ya watu
kupoteza maisha kutokana na magonjwa ya damu.
Amesema moja ya magonjwa hayo ni himofilia ambao husababisha damu kukosa uwezo wa kuganda inayosababishwa na ukosefu wa kiwango cha kutosha cha chembechembe za protini zinazotakiwa kugandisha damu, hali inayosababisha damu kuvuja kwa muda mrefu.
Amesema mgonjwa anayekumbwa na hali hiyo, endapo hatapata huduma ya haraka anaweza kupoteza maisha.
Dk Stella amesema Watanzania wengi hawana utamaduni wa kupima afya zao, jambo linalosababisha watoto wengi kupoteza maisha hasa wale wanaopelekwa kwa waganga kukatwa kilimi au kutahiriwa.
"Utakuta mzazi anampeleka mtoto kumtahiri au kukata kilimi hajui ana tatizo la himofilia au hana, mtoto anatokwa damu nyingi mpaka anapoteza maisha au wale ambao wanaishi karibu na hospitali wanampeleka hospitali ameshatokwa na damu nyingi," amesema.
Amesema kama kwenye familia kuna mtu ambaye alikuwa anatokwa na damu kwa muda mrefu, watoto wana uwezekano wa kurithi tatizo hilo ambalo ni himofilia, hivyo kabla ya kufanyiwa upasuaji wowote au hata kung'oa jino ni vizuri kupima uwezo wa damu kuganda.
Asilimia 97 ya wagonjwa wa himofilia hawajui kama wana ugonjwa huo na hawajawahi kupima.
Alisema wameshafanya mafunzo kwa waganga wa kienyeji wa jiji la Dar es Salaam pamoja na Pwani kuwafundisha ugonjwa huo, kwani watu wanaokwenda kwa waganga hao huchanjwa chale ambazo pia kama mtu ana himofilia anaweza kutoka damu mpaka akapoteza maisha.

No comments :
Post a Comment