Kamishna
Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea
Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya
kujitambulisha na kukuza mahusiano katika vyombo vya Ulinzi na Usalama
vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, (Kushoto) ni Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye.
NA MWANDISHI WA JESHI LA ZIMAMOTO
KAMISHNA
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye atembelewa na
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Phaustine Kasike mapema leo
asubuhi katika Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam. Lengo ni kujitambulisha na
kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili vya Ulinzi na Usalama.
Katika
ziara hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye,
alitumia fursa hiyo kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna Jenerali wa
Magereza na kumuahidi ushirikiano katika kulijenga Taifa.
Vilevile
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike amepata fursa ya kujifunza jinsi
gani Jeshi hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kufanya mazungumzo ya
kina na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo.
“Nimejifunza
mengi lakini pia nashukuru kwa kupata fursa ya kutembelea na kuona ni jinsi
gani tunaweza kushirikiana” alisema Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine
Kasike.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akisalimiana na Kamishna
Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike, baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
barabara ya ohio jijini Dar es Salaam.
No comments :
Post a Comment